Remix Tano Kali Zilizoachiwa na Rayvanny

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Neno ‘remix’ ni neno la kiingereza lenye maana ya kipande cha sauti ambacho kimebadilishwa kutoka kwenye uhalisia wake kwa kupunguzwa, kuongezwa au kubadilishwa baadhi ya sehemu kutoka kwenye toleo halisi la wimbo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Bob Junior Aachia ‘Itetemeshe’ Akimshirikisha Lava Lava [Video]

Kwenye muziki, nyimbo za remix zilianza na kupata umaarufu mkubwa huko nchini Jamaica kwenye miaka ya 60 na 70 baada ya Madjs na watayarishaji muziki kama King Tubby na Lee Scratch Perry kutokea nchini Jamaica kubadilisha midundo na miondoko halisi ya nyimbo ili kuweza kuvutia zaidi wasikilizaji.

Nchini Tanzania, remix zimekuwa maarufu sana na makala hii inaangazia remix tano ambazo msanii kutokea lebo ya WCB Rayvanny ameshawahi kushiriki na zikafanya vizuri:

Soma Pia: Diamond Platnumz Atangaza Ratiba ya Ziara yake ya Marekani

Number One Remix

Wimbo huu uliachiwa Februari 24 mwaka huu ukiwa umeandikwa na Rayvanny pamoja na msanii Enisa kutokea Brooklyn New York nchini Marekani huku Zest na Lizer Classic wakisimamia utayarishwaji wa ngoma hii. Kwenye kibao hiki, Enisa anachukua kipande za Zuchu ambaye alishirikishwa kwenye toleo la kwanza la wimbo huu na anapamba wimbo huu kwa mashairi mazuri ya lugha ya kiingereza. Kufikia sasa wimbo huu umetazamwa takriban mara Milioni 2 nukta moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=MbRkyXd4ohA

Tiptoe Remix

Kwa mara nyingine, Rayvanny alithibitisha kuwa muziki hauna mipaka baada ya Februari 19 mwaka 2018 kushirikishwa na msanii kutokea Florida nchini Marekani Jason Derulo kwenye ‘Tiptoe Remix’. Pamoja na kwamba ‘Tiptoe remix’ haina video, Rayvanny alipendezesha wimbo huu kwa kuimba kiswahili sanifu kilichochanganywa na kiingereza kwa mbali ili kunogesha wimbo huu ambao kufikia sasa umetazamwa mara laki sita tisini na mbili elfu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=3-iEiMsbbqo

Jeniffer Remix

Baada ya wimbo wa ‘Jeniffer’ kufanya vizuri sana, msanii Guchi hakuwa na hiyana bali kusafiri kutokea Nigeria hadi nchini Tanzania ili kuweza kukamilisha "Jennifer Remix" akimshirikisha Rayvanny. ‘Jeniffer Remix’ ni wimbo wenye vionjo vya Afro-pop na unaelezea zaidi changamoto wanazopitia wapendanao kwenye mahusiano hasa suala zima la udanganyifu kwenye mapenzi na kadhalika.

https://www.youtube.com/watch?v=2bXXaiwh1Zg

Fresh Remix

"Waambie mjini shule wasitamani vyote vimelipiwa. Kama ukipenda vya bure leta sahani utapakuliwa,” hiyo ni baadhi ya mistari aliyopita nayo Rayvanny kwenye wimbo huu uliotayarishwa na Tiddy Hoter huku maandalizi ya mwisho yakisimamiwa na Lizer Classic kutokea Wasafi Records.

https://www.youtube.com/watch?v=NGZLcnh8sto

Tetema Remix

Kutokana na ukubwa wa wimbo wa ‘Tetema’, Rayvannyna Diamond  waliungana na Patoranking pamoja na Zlatan wote kutokea nchini Nigeria kutoa ‘Tetema Remix’. ‘Tetema Remix’ ilipokelewa vizuri na mashabiki na kufikia sasa video ya wimbo huu imetazamwa mara milioni sita nukta tano kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=yOoqfaetRdc

Leave your comment