Nyimbo Mpya: Bob Junior Aachia ‘Itetemeshe’ Akimshirikisha Lava Lava [Video]

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Bob Junior ameachia wimbo mpya kwa jna ‘Itetemeshe’ akimshirikisha Lava Lava.

Kwenye wimbo huu, Bob Junior na Lava Lava wanamwagia sifa mwanamke mrembo na anayewapagawisha kutokana na miondoko yake ya kucheza.

Soma Pia: Nyimbo Mpya:Ngoma 5 Zilizoachiwa Bongo na Rayvanny, Marioo na Barakah the Prince

Bob Junior anatawala sehemu ya kwanza ya wimbo kwa kutumia sauti yake yenye umaridadi anaimba "Natoa nazidisha mbona bado jibu silipati maana umeshanimaliza umeniroga umeniweza wapi?"

Lava Lava anang'arisha sehemu ya pili ya wimbo kwa kutumia maneno ya kifasihi na sauti yake mujarab, Lava Lava anaimba : "Kwake macho yake yananitaka fundi saa kapoteza nati, msumari ghorofani kakanyaga mkandarasi (itetemeshe).

Soma Pia: Diamond Awaelimisha Wasanii Jinsi ya Kufanya Muziki wa Kimataifa

‘Itetemeshe’ imetayarishwa na KGT ambaye ni mtayarishaji wa muziki mkongwe hapa nchini Tanzania aliyehusika kutayarisha nyimbo kama ‘Nainai’ ya Ommy Dimpoz, ‘Cinderella’, ‘Nakshi Nakshi’ za Alikiba pamoja na wimbo uliobamba Tanzania nzima miaka kadhaa nyuma ‘Je Wajua’ wa Queen Darleen ambaye kwa sasa yuko Wasafi.

Aidha, video ya wimbo huu imefanyika visiwani Zanzibar ikiongozwa na Ivan ambaye ni mojawapo wa directors wakubwa sana wa muziki Tanzania.

Kwa muhtasari, Bob Junior ni mwanamuziki pia ni mtayarishaji wa muziki anamiliki studio yake ya Sharobaro Records iliyoweza kutengeneza nyimbo kali na zilizowafanya wasanii wengi wawe maarufu na miongoni mwa wasanii hao ni Diamond Platnumz.

Bob ndiye aliyetayarisha nyimbo za Diamond kama ‘Kamwambie’, ‘Mbagala’ na ‘Ntarejea’ ambazo zilimfanya Diamond awe maarufu.

Kufikia sasa video ya wimbo huu imetazamwa mara thelathini na moja elfu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=cMJ27cZc8W4

Leave your comment