Diamond Awaelimisha Wasanii Jinsi ya Kufanya Muziki wa Kimataifa

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki tajika kutoka Tanzania Diamond Platnumz amewahimiza wenzake katika tasnia ya muziki ya bongo kusoma soko za nchi za nje. Kupitia ujumbe aliyochapisha kwenya ukurasa wake wa Instagram, bosi huyo wa WCB alisema kuwa ni vizuri wasanii kujaribu aina tofauti za muziki iwapo wanataka kufanikiwa zaidi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘Sweet’ Akimshirikisha Guchi

Diamond Platnumz alisema kizazi cha sasa cha wasanii kina hofiya sana kujaribu vitu mbali mbali. Alieleza zaidi kuwa uoga wa wasanii ndio unaowazuia kuvuka hadi nyanja za kimataifa.

Kulingana na Diamond, wasanii wanafaa kufanya muziki wakilenga soko fulani ambalo ni la kigeni. Kufanya hivyo, Diamond alisema kutawawezesha kupata kipato zaidi na pia kuwapata mashabiki.

Aliongeza kuwa sio lazima msanii kuwaridhisha mashabiki wake wa nyumbani.

Soma Pia: Diamond Avimba Baada ya Wimbo wake 'Iyo' Kuvuma Afrika Kusini

"Kutolisoma soko na kuthubutu ndio kunawafanya vijana wengi kushindwa kuvuka kimataifa..na kuishia kuimba miziki ileile na kubakia palepale wakihofia kwamba wakiimbamiziki fulani, nyumbani hawatoipenda na watatukanwa...pasipo kujua kwamba kuna baadhi ya miziki wanatakiwa kuachia kwaajili ya ku target soko fulani na kuongeza mashaabiki na soko jipya... na sio kwa ajili ya kuridhisha watu wa nyumbani," Chapisho la Diamond mtandaoni lilisoma.

Taarifa yake Diamond ina uzito mwingi ikizingatiwa kuwa yeye ni mmoja wa wasanii wa kiafrika ambao wanavuma sana katika anga za burudani za kimataifa.

Hivi maajuzi Diamond alizuru Marekani ambapo alikutana na wasanii tajika mbali mbali.

Leave your comment