Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘Sweet’ Akimshirikisha Guchi

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Rayvanny ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Sweet’ akimshirikisha Guchi kutoka Nigeria.

‘Sweet’ ni wimbo wa mapenzi na kwenye kibao hiki, Guchi na Rayvanny kila mmoja anamsifia mwenzake kwa mapenzi wanayopeana huku wakisifiana kwa maneno matamu yanayokonga nyoyo za wasikilizaji.

Soma Pia: Diamond, Rayvanny, Marioo, Alikiba na Wasanii Wanaotarajiwa Kuachia Wimbo Mpya Wiki Hii

Guchi anafungua kibao hiki akiimba kwa sauti ya ndege mnana iliyonakiliwa kwa lugha ya kiingereza chenye lafudhi ya Afrika Magharibi : "If this is a dream baby I dont wanna wake up ooh, You give me life you give me vibe ooh, you be my energy I can’t deny oooh, superman you be my hero."

Rayvanny ametawala sana kwenye aya ya pili ya wimbo huu ambapo watu wengi wamedai kuwa amemuimbia mpenzi wake Paula.

Soma Pia: Nyimbo Tano Bora za Amapiano Zilizoachiwa na Wasanii Kutoka Bongo

"Bad bad katoto moto ni kiboko, magadigadi mboga mboga choroko, she call me dady dady nakapa joto my only one," aliimba Vanny Boy.

 Wimbo huu uliotayarishwa na Soundbwoi kwenye studio za Next Level Music unatarajiwa kuwa maarufu sana kwenye sherehe kama harusi na hafla tofauti tofauti.

Huu ni wimbo wa pili ambao Rayvanny ameshirikiana na Guchi, wa kwanza ukiwa ni Jeniffer Remix ambao video yake imetoka Julai 9 mwaka huu.

Kando na Guchi, Rayvanny anasifika kwa ushirikiano wake mzuri na wasanii wa kike kwani ameshafanya nyimbo na wasanii tofauti tofauti wa kike kama Queen Darleen, Zuchu, Enisa, Saida Karoli na Vanessa Mdee.

Kufikia sasa, video ya wimbo wa ‘Sweet’ umeshatazamwa takriban mara 90,000 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=ach6SBIUfs0

Leave your comment