Nyimbo Tano Bora za Amapiano Zilizoachiwa na Wasanii Kutoka Bongo

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Habari ya mjini sasa hivi ni muziki wa Amapiano. muziki huu ni wenye asili ya Afrika Kusini na ulianza kupata umaarufu mwaka 2012 na kutokana na umaarufu wake, majarida mbalimbali ya muziki duniani kama Billboard na Rolling Stone yamesifu sana muziki huu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Tano 5 Zinazotamba YouTube Tanzania Wiki Hii

Nchini Tanzania pia mambo yamekuwa sukari sana kwani wasanii mbalimbali wametengeneza nyimbo zenye mahadhi ya Amapiano ili waweze kwenda sambamba na dunia inavyotaka.

Makala hii inaangazia nyimbo 5 kali za Amapiano kutoka kwa wasanii watanzania

Mama Amina - Marioo ft Sho Madjozi & Bentley Smith

Ili kuweza kukidhi haja za mashabiki zake Marioo ilibidi asafiri mpaka Afrika kusini ili kutengeneza ‘Mama Amina’ na bila shaka safari yake ilizaa matunda kwani wimbo huu ulipendwa sana watu wa rika zote na ulikaa kwenye nafasi za juu kwenye chati mbalimbali za muziki hapa nchini Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=vJXB8kqKMOk

Soma Pia: Diamond Avimba Baada ya Wimbo wake 'Iyo' Kuvuma Afrika Kusini

Sandakalawe - Harmonize

Harmonize aliweka tabasamu kwa mashabiki wa muziki wake baada ya kuachia wimbo wa ‘Sandakalawe’ Juni 25 mwaka huu. Kwa Harmonize hakuitaji kwenda Afrika Kusini kukamilisha wimbo kwani ‘Sandakalawe’ ilitayarishwa na nguli wa muziki kutokea Tanzania Daxo Chali huku maandalizi ya mwisho yakifanywa, na Young Kiz Morento. Harmonize aliweka wazi kuwa yeye haoni shida kufanya muziki wa Amapiano kwani ni muziki wa kawaida na unawapa watu burudani.

https://www.youtube.com/watch?v=JWDTQdQgd4o

Iyo - Diamond Platnumz ft Focalistic, Mapara A Jazz & Ntoshi Gazi

Wiki kadhaa zilizopita, Diamond Platnumz aliamua kuonesha kuwa hamna aina ya muziki ambao hawezi kufanya kwa kuachia ‘Iyo’. Kwenye ‘Iyo’, Diamond Platnumz anarudisha watu vilabuni na sehemu za starehe kwani wimbo wote una mahadhi ya kuchezeka. Kufikia sasa, bado video rasmi ya wimbo huu haijatoka lakini inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=5WSdPi4toC4

Amapiano - Baba Levo

Baba Levo anaingia kwenye orodha ya wasanii kutoka Tanzania waliofanya ‘Amapiano’. Kwenye wimbo huu, Baba Levo ameshirikiana na mtayarishaji muziki aitwaye cBob Junior huku maandalizi ya mwisho yakiwa yamefanywa na Mocco Genius. Ukiachana na uchangamfu pamoja na mashairi mujarab ya wimbo huu, video ya ‘Amapiano’ imenakishwa na miondoko mbalimbali ya dansi ambayo huvutia kuangalia.

https://www.youtube.com/watch?v=DAChAmR-k8I

Mapopo - Damian Soul ft Nhlonipho

Imepita takriban miezi 7 tangu Damian Soul atoe ‘Mapopo’ lakini kila mara wimbo huu ukipigwa kwenye sherehe au hafla fulani bila hiyana watu husimama na kucheza. Kwenye ‘Mapopo’, Damian anatumia mdundo wa Amapiano akichanganya na baadhi ya maneno ya kiarabu ili kunogesha wimbo huo ambao ametunga na kuandika yeye mwenyewe.

https://www.youtube.com/watch?v=0kzQRY1H-kY

Leave your comment