Nyimbo Mpya: Video Tano 5 Zinazotamba YouTube Tanzania Wiki Hii

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ikiwa imeshatimia wiki ya mwisho ya mwezi Julai, tasnia ya muziki nchini Tanzania imezidi kuchangamka na kukua kutokana na wasanii kutoa kazi nyingi zenye ubora.

Soma Pia:Baba Levo Akashifu Harmonize Kwa Kumpa Anjella Gari Badala ya Kumpeleka Hospitali India

Zifuatazo ni nyimbo tano ambazo zimevuma sana au zinafanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube wiki hii.

Soma Pia: Diamond Avimba Baada ya Wimbo wake 'Iyo' Kuvuma Afrika Kusini

 Nimekuzoea - Nandy

The African princess anafungua pazia wiki hii baada ya kuachia video ya wimbo wake ‘Nimekuzoea’. Video hiyo imefanyika nchini Afrika Kusini na kuanzia miondoko ya dansi iliyotumika, mandhari, ubora wa picha hata stori ya video imevutia sana watazamaji. Kufikia sasa video ya wimbo huu imeshatazamwa takriban mara Milioni 2 nukta mbili kwenye mtandao ndani ya siku tano pekee.

https://www.youtube.com/watch?v=3I05z8Aa1BU

Ex wangu remix - Hamisa Mobetto × Seneta Kilaka

Sawa na wiki iliyopita, Hamisa Mobetto anaendelea kushikilia nafasi ya pili kwenye nyimbo zinazovuma kwenye mtandao wa YouTube nchini Tanzania. Wimbo huu umeonesha ni kwa namna gani Hamisa anaweza kubadilika na kufanya muziki wa aina yoyote na bila shaka umemuongezea mashabiki wengi.

https://www.youtube.com/watch?v=CmSgffQYaSo

Nyumba Ndogo - Zuchu

Sifa nyingi sana zimfikie DJ kidogodogo kwa kuweza kutayarisha wimbo huu ambao umemfanya Zuchu aendelee kutamba ndani na nje ya Tanzania. Kufikia sasa wimbo huu umetazamwa mara Milioni 6 nukta sita kwenye mtandao na hii inafanya ‘Nyumba Ndogo’ kuwa video ya pili ya singeli iliyotazamwa sana kwenye mtandao wa YouTube kwa hapa Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=KsU31FyvFxY

Jeniffer Remix - Guchi ft Rayvanny

Pamoja na kwamba anafanya muziki nchini Nigeria, msanii Guchi aliweka wazi kuwa anapenda sana muziki kutokea Tanzania na kwake yeye kufanya kazi na msanii Rayvanny ilikuwa ni kukamilisha ndoto yake ya muda mrefu. Kufikia sasa video ya ‘Jeniffer Remix’ iliyotoka tarehe Julai 9 mwaka huu imeshatazamwa mara Milioni 4 nukta moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=2bXXaiwh1Zg

Mtaalam - Mbosso

Kutoka kwenye albamu ya ‘Definition of Love’ tarehe 19 Julai mwaka 2021, Mbosso aliachia video ya ‘Mtaalam’ iliyoongozwa na Director Kenny kutokea Zoom Extra. Mbosso kwenye video hii anaonekana kufurahi na kula raha na mpenzi wake kwenye maeneo mbalimbali. Kufikia sasa video ya wimbo huu ishatazamwa mara Milioni moja nukta tisa kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=giHgGzX2PAI

Leave your comment