Diamond Avimba Baada ya Wimbo wake 'Iyo' Kuvuma Afrika Kusini

[Picha: Diamond Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtindo wa muziki wa Amapiano unavuma sana nchini Tanzania huku wasanii wengi wakionekana kuuiga. Baadhi ya wasanii wakubwa wa Bongo Flava wameimba kutumia mdundo wa Amapiano japo kwa lugha ya Kiswahili.

Diamond Platnumz kwa sasa anatamba sana mtandaoni kupitia wimbo wake wa ‘Iyo’ ulioimbwa kwa mtindo wa Amapiano. Kwenye ngoma hiyo Diamond alishirikisha wasanii wa Afrika Kusini ambao ni Focalistic , Mapara A Jazz na Ntosh Gazi.

Soma Pia: Diamond Platnumz na Rayvanny Wadokeza Ujio wa Wimbo Wao Mpya

Ngoma hiyo imevuma sana hadi Afrika Kusini na mashabiki wengi wameirekodi wakisakata densi ya ‘Iyo’. Diamond alichapisha baadhi ya video hizo kutoka kwa mashabiki kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Katika moja wapo ya video iliyo waonyesha watu kutoka Afrika Kusini wakisakati densi ya ‘Iyo’, Diamond alichapisha ujumbe ambao umezua hisia tofauti. Kwenye ujumbe huo Diamond Platnumz alionekana kana kwamba anavimba kwa sababu ya ngoma yake kupokea mapokezi mazuri.

Soma Pia: Nyimbo Tano Kali Kutoka Tanzania Ambazo Zimekosa Video

Bosi huyo wa WCB alisema kuwa wasanii wengine walikuwa wanaimba kupitia mtindo wa Amapiano ile ngoma zao hazikuvuma kwa kiasi cha kufika Afrika kusini.

"Mnapoimbaga hivi vinyimbo, basi Walau jitahidini na wenyewe ziwafikie," ujumbe wa Diamond kwenye mtandao wa Instagram ulisoma.

Wadau mbali mbali katika tasnia ya burudani wameeleza kuwa ujumbe huo huenda ulikuwa umeelekezwa kwa Harmonize kwani yeye pia alishiriki katika kutoa nyimbo za Amapiano.

Aidha Harmonize pia hivi karibuni anatarajiwa kuachia ngoma nyingine ya Amapiano. Wimbo wake wa ‘Sandakalawe’ uliochukuwa mtindo wa Amapiano pia ulitamba sana mtandaoni licha ya kukumbwa na kashfa ya ununuzi wa watazamaji.

Leave your comment