Diamond Platnumz na Rayvanny Wadokeza Ujio wa Wimbo Wao Mpya

[Picha: Grammy]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii kutokea lebo ya WCB Diamond Platnumz pamoja na Rayvanny wameonjesha mashabiki kipande kidogo cha wimbo wao ambao bado upo kapuni. Kupitia akaunti yake ya Instagram yenye wafuasi Milioni 12 kwenye sehemu ya Instastory, Diamond Platnumz amechapisha video hiyo ikimuonesha Rayvanny akirekodi wimbo huku sauti ya wimbo huo ambao bado haujatoka ikiwa inasikika.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Mpya za Zuchu, Nandy na Anjella Zinazovuma Bongo Wiki Hii

Mara zote, Diamond Platnumz na Rayvanny huleta kazi bora pale ambapo wao hushirikiana kwa pamoja. Wasanii hawa wanaofanya vizuri Tanzania wameshafanya nyimbo kadhaa kama ‘Tetema’ , ‘Vumbi’, ‘Amaboko’ pamoja na ‘Mwanza’.

Kwa siku za hivi karibuni, Diamond Platnumz ameonekana kutumia akaunti yake ya Instagram kuonjesha mashabiki zake ni kitu gani anaandaa kwani wiki tano zilizopita alichapisha video kwenye instagram akiwa kwenye gari na mrembo huku akiimba kionjo cha wimbo uliopachikwa jina la loyal na mashabiki.

Sambamba na hilo, kwenye safari yake ya Marekani alipokwenda kwa ajili ya tuzo za BET na maandalizi ya albam amekutana na wasanii kama Wiz khalifa, Busta Rhymes, Snoop Dogg na mtayarishaji muziki Swizz Beats ambaye ana ukaribu mkubwa na Diamond Platnumz.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond Aachia ‘Iyo’ Akiwashirikisha Focalistic, Mapara A Jazz na Ntoshi Gazz

Kwa sasa, Diamond Platnumz anaungana na wasanii kama Nandy, Marioo, Whozu, Country Boy, Ibraah, Kili, Alikiba, Harmonize pamoja na Beka Flavour ambao wameweka wazi kuwa wako mbioni kuachia albam.

Leave your comment