Nyimbo Mpya: Video Mpya za Zuchu, Nandy na Anjella Zinazovuma Bongo Wiki Hii

[Picha: Mzigo TV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwezi Julai ndio huu unazidi kukatika na mashabiki wa muziki kutokea nchini Tanzania wameendelea kuwapa ushirikiano wasanii kwa kusikiliza muziki kwenye majukwaa tofauti tofauti ikiwemo YouTube. Ukweli ni kwamba pamoja na nyimbo nyingi kuachiwa wiki hii, zifuatazo ni nyimbo tano ambazo zinavuma sana kuliko nyimbo nyingine zote kwenye mtandao wa YouTube nchini Tanzania.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond Aachia ‘Iyo’ Akiwashirikisha Focalistic, Mapara A Jazz na Ntoshi Gazz

Nyumba Ndogo – Zuchu

Akiiwakilisha vyema bendera ya WCB, mwanadada Zuchu kwa wiki ya tatu mfululizo ameendelea kushika usukani kwa kuwa namba moja kwenye mtandao wa YouTube. Kufikia sasa ‘Nyumba Ndogo’ ambayo video yake ilitoka Julai mosi mwaka huu imeshatazamwa mara Milioni 5 nukta tano na idadi hiyo inategemewa kuongezeka kadri siku zinavyoenda.

https://www.youtube.com/watch?v=KsU31FyvFxY

Ex Wangu Remix - Hamisa Mobetto

Mobetto anasema mara ya kwanza kusikia wimbo wa ‘Ex Wangu’ ni kwa rafiki yake aishie Oman na ndipo hapo akachukua uamuzi wa kumtafuta Seneta Kilaka kwa ajili ya kufanya Remix ambayo imeweza kufanya vizuri sana. Ikiwa ni wiki ya pili mfululizo kushika namba mbili video ya ‘Ex wangu remix’ iliyotoka tarehe 1 Julai, kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 1 nukta saba kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=CmSgffQYaSo

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Chege Amshirikisha Ommy Dimpoz Kwenye Wimbo Mpya ‘Show Time’

Nimekuzoea - Nandy

Utofauti aliouonesha Nandy kwenye kazi hii umefanya yeye kuonekana kama mwanamuziki ambaye ameanza muziki siku chache zilizopita. Nani alitegemea Nandy kuigiza kama mwanafunzi wa shule? Kufikia sasa video hii ya ‘Nimekuzoea’ iliyoachiwa Julai 14 imetazamwa mara Milioni 1 nukta nne huku watu thelathini na tano elfu wakionesha kupenda video hii kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=3I05z8Aa1BU

Jeniffer Remix - Guchi ft Rayvanny

Mengi yalitarajiwa baada ya Guchi kuja jijini Dar Es Salaam ili kufanya kazi na Rayvanny na bila shaka "Jeniffer Remix" imeonesha safari ya Guchi kutokea Lagos mpaka Dar ilizaa matunda. Kwenye upande wa YouTube video hii yenye siku 11 tu tangu kuachiwa kwake imeshatazamwa mara milioni 3 nukta moja huku pongezi za kutosha zikielekezwa kwa Eris Mzava ambaye ndiye alihusika kuongoza video hii.

https://www.youtube.com/watch?v=2bXXaiwh1Zg

Sina Bahati - Anjella

Kutokea lebo ya Konde Gang Anjella kwenye ‘Sina Bahati’ anawakilisha watu wote ambao washawahi kukimbiwa na wapenzi wao waliowaamini. Kitu kilichovutia watu kuhusiana na video hii ni hadithi nzuri iliyopangiliwa, uhalisia uliopo pia uwepo wa mwanamitindo Calisah ulinogesha zaidi video hii ambayo kufikia sasa imetazamwa mara Milioni 1 nukta nne lwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=dfb_TG4eUSo

 

Leave your comment