Nyimbo Mpya: Chege Amshirikisha Ommy Dimpoz Kwenye Wimbo Mpya ‘Show Time’

[Picha: Chege Chigunda Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Chege Chigunda ametoa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Show Time’.

‘Show time’ kama jina linavyojieleza ni wimbo wa kuchezeka ambao unategemewa kubamba sana kwenye kumbi za starehe na klabu mbalimbali hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Soma Pia: Babu Tale Aeleza Mbona Diamond Alikosa Tuzo la BET

Wimbo huu umetengenezwa na mtayarishaji nguli wa muziki nchini Tanzania Genius Jini na Chegge amemshirikisha msanii Ommy Dimpoz kwenye wimbo huu.

Mara tu baada ya kuachiwa mtangazaji maarufu nchini Tanzania Lil Ommy alijirekodi akiwa anacheza wimbo huo ambao kufikia sasa umetazamwa takriban mara elfu mbili kwenye mtandao wa YouTube.

‘Show Time’ ni wimbo ambao Chege ametumia sana Lugha ya picha pamoja na tafsida. Katika aya ya kwanza ya wimbo huu, Chege anashawishi mtoto wa kike wacheze pamoja kwani wenzake waNgefurahi sana kupata nafasi hiyo.

Soma Pia: Marioo Atangaza Tarehe ya Kuachia Albamu Yake Mpya

"Leo si siku ya Simba kucheza na mimi ukinipa mwenzako ntaweza, mguu juu ya kitanda mwingine juu ya meza. Usitupe nanga ukaikata kuna wengine wanaitaka kuna mwajuma kaja na dela fatuma kaja na Kanga,"aliimba Chege.

 Kwenye aya ya pili baada ya kiitikio cha wimbo, Chege anamuelekeza mpenzi wake kwa vitendo namna ya kucheza vizuri. "Inama shika mabega ipepete onyesha figure ukinipa yote shega usibane kipapatio nataka kula ka kwio."

Wimbo huu unakuja kipindi ambacho Chege anatarajiwa kutoa video zaidi kutoka kwenye EP yake ya ‘Burudani’ iliyotoka mwanzoni mwa mwaka huu.

EP ya Burudani ilisheheni nyimbo sita na imehusisha wasanii kama Baddest 47 kwenye "Story" huku wasanii wengine ni pamoja na Rosa Ree, Genius na Mabantu.

https://www.youtube.com/watch?v=UJaHfLjrNa8

Leave your comment