Marioo Atangaza Tarehe ya Kuachia Albamu Yake Mpya

[Picha: Marioo Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki na mwandishi nguli kutokea nchini Tanzania Marioo ametangaza kuwa albamu yake mpyaitatoka rasmi tarehe 25 Septemba mwaka 2021.

Soma Pia: MB Dogg Aeleza Changamoto Anazopitia Katika Harakati za Kurejea kwa Muziki

"Im so happy nimejua tarehe ya albamu yangu kutoka 25/9/2021. I can't wait. Hivi unahisi itaitwaje?" alisema Marioo.

Tetesi za Marioo kuachia albamu zilianza mapema mwaka huu. Wiki chache zilizopita, aliyekuwa meneja wa Marioo D'fighter kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka wazi kuwa albamu ya Marioo ipo tayari na ni suala la muda tu waiachie albamu hiyo.

Taarifa za Marioo kutoa albamu zinakuja kipindi ambacho wasanii wengi wa Bongo Flava wameweka wazi kuwa wako mbioni kuachia albam, wasanii kama Diamond platnumz, Alikiba, Harmonize, Whozu, Country Wizzy, Killy na Young Lunya wameshatangaza kuwa albam zao zipo tayari.

Soma Pia: Zuchu Azungumzia Mafanikio Yake Mwaka Mmoja Kwenye WCB

Sambamba na taarifa hiyo, Marioo hajaweka wazi jina la albam au ni wasanii gani ambao watashirikishwa kwenye albamu hiyo ambayo inategemewa kuachiwa Septemba.

Mara ya mwisho kwa Marioo kuachia wimbo ilikuwa ni mwezi Machi mwaka huu pale ambapo alitoa ‘For You’, wimbo uliotayarishwa na Abbah Process huku video ya wimbo huo imetengenezwa na Director Adam Juma na kufikia sasa ishatazamwa takribani mara Milioni 2 nukta moja kwenye mtandao wa YouTube.

Leave your comment