MB Dogg Aeleza Changamoto Anazopitia Katika Harakati za Kurejea kwa Muziki

[Picha: MB Dogg Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram   

Msanii mkongwe kutoka Bongo MB Dogg amezungumzia safari yake ya kurejea kwenye muziki na changamoto ambazo anakabiliwa nazo hasa katika muziki wa kizazi kipya. MB Dogg alichapisha taarifa kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii ambapo alieleza kuwa baadhi ya nyimbo zake zimefutwa kutoka mtandao wa YouTube na kufadhaisha juhudi zake za kutengeneza nyimbo.

Soma Pia: Country Boy Atangaza Kukamilika Kwa Albamu Yake Mpya

Kulingana na MB Dogg, nyimbo zake pia zinauzwa mkondoni bila yeye kufaidika na kipato.

"Lakini hata niliporudi mwaka 2015 na kuwa chini ya QS J mhonda Boss vita bado iliendelea nia ni kunipoteza kabisa kwenye muziki wa kizazi kipya. 2020 kurudi tena kwenye muziki lakini bado nakutana na changamoto ngumu zaidi. Nyimbo zangu kuuzwa kwenye majukwaa ya kidigital bila ridhaa yangu. Nimewatafuta wahusika lakini bado hawaonyeshi ushirikiano wowote ni takribani mwaka sasa wananikimbia kwa ahadi za uongo ambazo hazitekelezeki nimeamua kutumia busara miezi yote hiyo kwa kutaka suruhu kwa amani lakini hawaonyeshi dalili ya kujali chochote nimepita kwenye mamlaka husika cosota na kujaribu kukaa nao mezani lakini bado wanaleta dharau sana roho inaniuma sana ubunifu wangu kuwekwa madukani na kisha watu wengine kunufaika bila mimi kujua wala kunijali kwa chochote," chapisho la MB Dogg lilisoma.

MB Dogg alikuwa mwanamuziki mwenye ushawishi mkubwa takriban mwongo mmoja Iliyopita. MB Dogg wakati wake alivuma na kutamba kupitia ngoma kama vile Si Uliniambia, Natamani, na zingine nyingi.

 

Leave your comment