Country Boy Atangaza Kukamilika Kwa Albamu Yake Mpya

[Picha: Yinga]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii kutokea Konde Music Worldwide Country Boy amesema kuwa albamu yake ya pili tangu aanze muziki ipo tayari.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

Country Wizzy ambaye siku chache zilizopita alitoa wimbo wake ‘Hiphop’ ameweka wazi kuwa albamu yake imeshakamilika na ni suala la muda tu mpaka aiachie.

"Sipendi kuongeza idadi ya watu ambao wanahaidi, to say it moja kwa moja kwamba albamu iko tayari na iko tayari muda mrefu because me ni mtu ambae nafanya kazi sana so albamu yangu ipo ready ni albamu ya kipekee sana ikifika muda wake ntawaambia," alieleza Country.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano za Zuchu, Diamond, Alikiba na Rayvanny Zinazovuma YouTube

Kutokea label ya Kondegang Country Wizzy anakuwa ni msanii wa tatu kuweka wazi kuwa kashakamilisha albamu yake.

Akiongea kwenye ‘Simulizi na Sauti’, msanii Killy aliweka wazi kuwa albam yake ipo tayari lakini Harmonize, ambaye pia ndiye mkurugenzi mtendaji wa label hiyo aliweka wazi albam yake iitwayo ‘High School’ itatoka hivi karibuni.

Kuhusiana na jina la albamu hiyo Wizzy alisema "Ntatamani kuwaambia the name of the album lakini nitawafahamisha as soon as possible lakini album iko ready na album hii inaenda kuwa ya kipekee na tofauti kabisa, sio yule Country ambaye mnaweza mkamuimagine, ni albam kubwa sana."

Taarifa hii kutoka kwa Wizzy inakuja mwaka mmoja na miezi kadhaa baada ya msanii huyo kuachia ‘Yule Boy’ Tarehe 15 Novemba 2020 ikiwa ni albam iliyosheheni nyimbo 31 alizoshirikiana na wasanii kama Harmonize, Mwana Fa, Khaligraph Jones, Jolie, Moni Centrozone, Young Lunya na wengineo.

Kando na Country Wizzy wasanii wengine kama Alikiba, Diamond Platnumz, Harmonize, Killy, Marioo, Nandy, Whozu na wengineo wengi wako mbioni kuachia albamu zao.

Leave your comment