Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii
13 July 2021
[Picha: The Citizen]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Soko la muziki nchini Tanzania limeendelea kukua kwani wasanii wameendelea kutoa kazi kila kukicha na wiki hii mambo hayajakuwa tofauti sana kwani wasanii Hamisa Mobeto, Aslay, Bright Music, Killy na wengineo wameendelea kuendeleza utaratibu huo.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Hamisa Mobetto Aachia Wimbo Mpya ‘Ex Wangu’ [Video]
Zifuatazo ni ngoma tano kali zilizotoka wiki hii:
Mwisho – Killy
Wimbo wa pili kutokea kwa Killy tangu alipotia wino kwenye label ya Konde Gang. Bila shaka, Killy ameendelea kuonesha kuwa yeye bado ni fundi wa kuandika nyimbo za mapenzi. kufikia sasa, wimbo huu umetazamwa mara milioni moja nukta saba kwenye mtandao wa YouTube.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lulu Diva, Lava lava Waachia Wimbo Mpya ‘Samahani’ [Video]
Shangingi Mtoto - Aslay
Baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kutoa wimbo, Aslay anarudi kwa kishindo na wimbo wake wa ‘Shangingi Mtoto’. Kwenye wimbo huu, Aslay ambaye ni maarufu kwa uandishi wa nyimbo za mapenzi humu anaelezea jinsi watu wanavyofanya maamuzi hasi maishani hivyo kuwagharimu.
Demu Wangu - Bright ft Meja Kunta
Muziki wa Singeli umeendelea kushika kasi nchini Tanzania kwani msanii Bright nae ameamua kushirikiana na Meja Kunta kwenye wimbo huu ambao umetoka siku sita nyuma.
Ex Wangu Remix - Hamissa Mobeto ft Seneta Kilata
Mwanamuziki Hamissa mobetto ameendelea kuonesha kuwa muziki hauna mipaka baada ya yeye kuamua kufanya muziki aina ya singeli. Akishirikiana na Seneta Kilata, Mobetto ameonesha umaridadi mkubwa kwenye wimbo huu ambao mpaka sasa video yake imetazamwa mara milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.
Imoo - Frida Amani ft Mimi Mars
Ni muziki mzuri tu unatokea pale ambapo wasanii wawili wakike wanapoamua kushirikiana kutengeneza wimbo. ‘Imoo’ ni wimbo wenye miondoko ya Hip-hop na mdundo wa kuchezeka na kama kawaida Frida Amani amechana huku Mimi Mars akifanya kiitikio cha wimbo huu. Wimbo huu hauna video rasmi bado lakini inategemewa itaachiwa hivi karibuni.
Leave your comment