Nyimbo Mpya: Lulu Diva, Lava lava Waachia Wimbo Mpya ‘Samahani’ [Video]

[Picha: Lulu Diva Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Lulu Diva ameachia wimbo mpya uitwao ‘Samahani’ akimshirikisha Lava lava.

Wimbo huu umetengenezwa na mtayarishaji muziki maarufu nchini Tanzania Gachi B huku maandalizi ya mwisho ya wimbo huo yamefanywa na Lizer Classic kutokea Wasafi Records.

Kwenye ‘Samahani’, Lulu anaonesha ni vitu gani ambavyo vinamkwaza kwenye maisha ya kila siku kama umbeya, kukosa uaminifu kwenye mahusiano, uongo, roho mbaya na mengineyo mengi huku akitumia neno ‘Samahani’ kufikisha ujumbe.

Soma Pia: Lulu Diva Amsifu Zuchu Kwa Kuwa Moja wa Wasanii Bora Tanzania

Kwenye aya ya kwanza Lulu anaimba "Samahani sihitaji kushare, samahani sitaki mbeya, samahani nawakosea hivi kweli mtaoana au nawafokea." Anaongeza kwa kuimba "Nikiwa na pesa kama nawakwaza, kama kudanga kwani mi wa kwanza, nitakulipa kwani mi kwanza"

Lava lava anatawala aya ya pili wa wimbo huu akizungumzia mapenzi na mojawapo ya mstari ambao uligusa hisia za watu wengi ni pale Lava lava alipoweka wazi hisia zake kwa Lulu Diva akiimba : "Samahani Lulu nakupenda kiukweli siwezi kuficha ndio maana ulivyonipa denda video zetu nikazivujisha"

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lulu Diva Aachia Ngoma Mpya Kwa Jina ‘Mama' [Video]

Wimbo huu umezua taharuki kubwa mtandaoni hasa kwenye ukurasa wa Instagram na akaunti ya YouTube ya Lulu Diva ambapo mashabiki wamehoji kama ugomvi wake na Lava lava kwenye kipindi cha Lavidavi cha Diva the boss ilikuwa ni kiki tu kwa ajili ujio wa wimbo huo.

Sambamba na audio, Lulu Diva ameachia video ya wimbo huu iliyoongozwa na Joowzey na video hii ndani ya masaa mawili ilikuwa ishatazamwa mara 16,000 kwenye YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=z3ctoCgs3PE

Leave your comment