Lulu Diva Amsifu Zuchu Kwa Kuwa Moja wa Wasanii Bora Tanzania

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii kutoka Tanzania Lulu Diva amejitokeza kumsifia mwanamuziki wa WCB Zuchu kwa kuwa miongoni mwa watumbuizaji bora wa kike katika tasnia ya burudani ya Tanzania. Lulu Diva alikuwa akiongea kupitia taarifa ambayo alichapisha kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii ambapo alidai kuwa wanamuziki wengi wa kike walikuwa wakififia.

Soma Pia: Nyimbo Mpya : Zuchu Aachia ‘Nyumba Ndogo’, Ngoma Mpya ya Singeli

Hata hivyo, aliendelea kusema kuwa Zuchu alikuwa mwanamuziki mashuhuri wa kike nchini Tanzania kwa kujitolea kwake na bidii katika muziki. Lulu Diva alisema kuwa kuna uwezekano kwamba Zuchu sio mwanamuziki bora zaidi wa kike nchini Tanzania, ila kujitolea kwake kumemfanya awe mfano mwema miongoni mwa wasanii wa kike.

Mwimbaji huyo alidai kuwa wasanii wengi wa kike nchini Tanzania hawawezi kuburudisha hadhira. Kulingana na Lulu Diva, mwanamuziki mwingine wa kike ambaye angeweza kufikia kiwango cha Zuchu alikuwa Shaa.

Soma Pia: Diamond Platnumz Atangaza Kuachia Wimbo Mpya Hivi Karibuni

"Inawezekana Zuchu sio msanii bora alikuwa kike (kwenye kuimba) ila daaah, anajitahidi kutoa burudani. She can entertain maan, kitu ambacho wasanii wengi wa kike bongo hawana, alikuwepo mmoja tu Shaa," Lulu Diva alisema.

Zuchu ameibuka kuwa miongoni mwa wanamuziki wakuu wa Tanzania katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja tangu aanze katika tasnia ya muziki kupitia rekodi za WCB. Wachambuzi wamesema kuwa lebo ya rekodi ya WCB ilichangia pakubwa katika kufanikiwa kwa Zuchu.

Leave your comment