Nyimbo Mpya : Zuchu Aachia ‘Nyumba Ndogo’, Ngoma Mpya ya Singeli

[Picha: DJ Mwanga]

Mwandishi: Omondi Otieno

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Zuchu ameaachia wimbo mpya wa SIngeli kwa jina ‘Nyumba Ndogo’.

Wimbo huu una mdundo wa kasi na unazungumzia kisa cha mwanamke ambaye bwanake ameoa bibi wa pili.

Kwenye wimbo huu, Zuchu anachukua nafasi ya ‘Nyumba Ndogo’  kwa jina lingine ‘Mwanamke wa Pili’.

Anaeleza kuwa bwanake amekuwa akilalamika kwamba bibi yake wa kwanza hajawajibika hasa katika kuanda chakula na kumlinda yeye kama mumeo.

“Yamenifika kwa koo! We mwanamke mwenzangu…Bwana ako analalamika kila akija nyumbani, eti hujui kupika, kula kwako hatamani, kwangu lakipenda tembele toto laini laini… Nimemganda mumeo kama kichwa na kisogo…,” Zuchu aliimba.

Wimbo huu umetengezwa na DJ Kidogodogo, huku matayarisho ya mwisho yakifanywa na Lizer.

‘Nyumba Ndogo’ imepokelewa vizuri na inazaidi ya watazamaji elfu ishirini kwenye YouTube dakika chache baada ya kuachiwa.

Video rasmi ya ngoma hii bado haijachiwa, lakini ripoti zinaeleza kuwa itakuwa ikiachiwa hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=rqe-0SpJfCY

Leave your comment