Nyimbo Mpya: Lulu Diva Aachia Ngoma Mpya Kwa Jina ‘Mama' [Video]

[Picha: Lulu Diva Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa bongo Lulu Diva ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Mama’.

Katika wimbo huu, Lulu anamuimbia mamake ambaye ameugua kwa muda sasa. Katika hali ya majonzi na uchungu Diva anatumai kuwa mamake atapata nafuu hivi karibuni ilia pate kufurahia umaarufu aliopata katika usanii wake.

Diva anelezea jinsi mamake alibaki kumlea baada ya baba yake kuaga . Mistari ya wimbo huu yana uchungu na majonzi mengi akitamani mamake arudishe fahamu yake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021

“Hii ni kutoka moyoni nakupenda mama, na ndio sababu kutwa mwanao napambana, Kinacho ni tesa moyoni unaumwa ila naamini ipo siku utapona…” aliimba Diva.

Katika video hii, Lulu amemhusisha mamake na yeye mwenyewe anavyong’ang’ana kila siku kumlea mamake mzazi.

Mamake Lulu amekua mgonjwa kwa muda na wimbo huu ni kwa kuwashukuruku kina mama wote ulimwenguni kwa kulea wana wao.

Soma Pia: Tembo Vs Chui: Harmonize, Rayvanny Waachia Nyimbo Mpya ‘Vibaya’ na ‘Nyamaza’

Video hii imetengezwa kwa ufundi mkubwa huku mavazi yaliyovaliwa pia yakiwa ya mitindo tofauti.

Vilevile, katika wimbo huu, Lulu anawasifia kina mama wengine wa Tanzania kama rais wa Muungani wa Tanzania Bi.Samia Suluhu, Mbunge wa Tanga Bi. Ummy Mwalimu na hata Mama Dangote.

Kufikia sasa, wimbo huu unaendelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube na watazamaji zaidi ya elfu sitini.

Mdundo wa wimbo huu ulitengezwa na Kimambo na kuandikwa na Wyse Tz .

https://www.youtube.com/watch?v=BtJFyurZNAM&ab_channel=LuluDiva

Leave your comment