Zuchu Azungumzia Mafanikio Yake Mwaka Mmoja Kwenye WCB

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Zuchu ameeleza kuwa mafanikio yake mwaka mmoja tangu kujiunga na WCB inadhihirisha kuwa amefanya kazi kwa bidii ili kufikia hapo alipo sasa.

Alitoa mfano wa mafanikio ya jinsi amepata watazamaji zaidi ya milioni mia mbili kwenye mtandao wa YouTube. Aidha mwimbaji huyo pia alifunua kuwa hakujua kuwa atakuwa na ushawishi mkubwa na nyimbo zake kusikilizwa kote barani Afrika.

Soma Pia: Zuchu Aweka Rekodi Mpya, Afikisha Jumla ya Watazamaji Milioni Mia Mbili Kwenye YouTube

Zuchu ambaye amesainiwa chini ya WCB aalielezea furaha na jinsi nyimbo zake zilivyopokelewa na mashabiki wakiwemo watoto wadogo.

"Jitihada zinalipa. Kwa sababu namba haziongopi. Huezijifananisha na watu. Lkkini ukiona kwenye walimo nawe umo, basis ina maana unafanya vizuri. Tofauti ya mwaka kabla nikitoka, mini nilikuwa bado mwanamuziki napambania sanaa. Lakini wewe ulikuwa hunijui, lakini sasa hivi tuko hapa. Kwa hivyo zile namba zinaonesha pia muitikio. Ebu nikupe mfano mmoja, mini sikuwahi kutarajia kuwa nitaenda mkoa kama Chatu na watoto wanijue, lakini unaenda unaenda mkoani na huko ndani ndani ambako utasema huku ata mimi sitoboi, lakini unapata watoto wanakuimbia sukari," Zuchu alieleza.

Hivi majuzi, Zuchu aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kike wa kwanza emeo la Afrika Mashariki kufikisha watazamaji milioni mia mbili kwenye YouTube. Pia yeye ndio msanii wa kike aliye na video iliotazamwa zaidi YouTube Tanzania.

Leave your comment