Babu Tale Aeleza Mbona Diamond Alikosa Tuzo la BET

[Picha: Nairobi News]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Meneja wa muda mrefu wa mwanamuziki Diamond Platnumz Babu Tale kwa mara ya kwanza ameeleza sababu ya msanii wake kukosa tuzo ya BET inayoandaliwa na kituo cha Black Entertainment Television.

Soma Pia: Zuchu Azungumzia Mafanikio Yake Mwaka Mmoja Kwenye WCB

Akifanya mahojiano na kituo cha Dizzim, Babu Tale alieleza kuwa kukosa wawakilishi kutokea Tanzania kwenye kamati ya BET ilikuwa ni mojawapo ya sababu ya Diamond kuondoka mikono mitupu.

"BET wanaopiga kura ni watu wa Academy wenyewe watanzania hakuna mtu hata mmoja anaepiga kura BET, Kenya yuko mmoja, Nigeria wako more than 10 we unashinda vipi?" alieleza meneja huyo.

Babu Tale alieleza pia kuwa kitendo cha Diamond kutajwa kuwania kipengele hicho ni ushindi tosha kwani tofauti na washindani wenzake aliokuwa anawania nao kwenye kipengele hicho, Diamond anaimba kiswahili, lugha ambayo wazungu wengi hawaijui.

Soma Pia: MB Dogg Aeleza Changamoto Anazopitia Katika Harakati za Kurejea kwa Muziki

“Watu wanatakiwa wajue sisi tunaimba Kiswahili wenzetu wanigeria wanaimba kizungu, sisi tunaoimba vile (kiswahili) tunashindana na watu wanaimba lugha ya dunia ndo maana tunaenda na slogan yetu ya Swahili Nation, tunataka kuona kuwa tukiwa tunakutana na mzungu tunaimba nae Kiswahili," Tale alidokeza.

Aidha, Tale aliweka bayana kuwa Diamond Platnumz na uongozi wote wa Wasafi walijua fika kuwa hawatoshinda tuzo hiyo ila kilichofanya washiriki kwenye hafla hiyo ni kutengeneza mtandao na wasanii wakubwa nchini marekani pamoja na kumalizia albamu ya Diamond Platnumz.

Kuhusiana na vazi la kimasai alilovaa Diamond Platnumz kwenye hafla hiyo, Tale alisema "Angalia aliyepewa tuzo na aliyekosa tuzo nani ametrend kimavazi kwenye mitandao. Its a strategy. Lazima tupate kuzungumziwa kwenye red carpet, next time watakwenda kututazama wakitusoma watakwenda kujua kiasi gani tuna nguvu Afrika na Afrika Mashariki kiujumla."

Leave your comment