Nyimbo Mpya: Diamond Aachia ‘Iyo’ Akiwashirikisha Focalistic, Mapara A Jazz na Ntoshi Gazz

[Picha: Diamond Platnumz]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Diamond Platnumz ameachia wimbo mpya wenye jina ‘Iyo’ akishirikiana na rapa kutokea Afrika kusini Focalistic, Mapara A Jazz pamoja na Ntoshi Gazz.

Soma Pia: Snoop Dogg Amshauri Diamond Jinsi ya Kuwa Bora Kimuziki

‘Iyo’ ina vionjo vya Amapiano na imetayarishwa na Salmini Maengo almaarufu kama S2kizzy kutokea Pluto huku maandalizi ya mwisho yamefanywa na Lizer Classic kutokea Wasafi records.

Kwenye wimbo huu, Diamond anawarudisha watu vilabuni kama ambavyo alifanya kwenye ‘Kamata’.

Wimbo huu unategemewa kufanya vizuri sana kwenye sherehe na kumbi mbalimbali za starehe kwani una mahadhi ya kuchezeka kama ambavyo muziki wa Amapiano ulivyo. Kwenye kiitikio Diamond Platnumz anaimba "Godoro tumeweka maji, sisi tunakesha" akimaanisha kuwa wako tayari kukesha kwa ajili ya kufanya sherehe na kufurahi.

Soma Pia: Zuchu Aweka Rekodi Mpya, Afikisha Jumla ya Watazamaji Milioni Mia Mbili Kwenye YouTube

Kufikia sasa wimbo huu umetazamwa takribani mara elfu thelathini na tano ndani ya nusu saa tu.

Wimbo huu unakuja siku 21 baada ya Diamond Platnumz kuachia wimbo wake wa ‘Kamata’.

 Walioshirikishwa kwenye wimbo huu ni Focalistic ambaye ni rapa kutokea Afrika Kusini. Focalistic ameshafanya kazi na wasanii wakubwa barani Afrika kama Davido kwenye ‘Ke Star Remix’ pamoja na Cassper Nyovest.

Pia Mapara A Jazz kundi la muziki kutokea Afrika kusini limeshiriki kwenye wimbo huu. Kundi hilo lilianza mwaka 2007 na limesheheni vijana wawili Lenny Sbechu pamoja na Man Malaya ambao sauti zao zimesikika kwenye wimbo huu.

Kufikia sasa bado haijafahamika kama wimbo huu utakuwepo kwenye albamu yake Diamond ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=5WSdPi4toC4

Leave your comment