Diamond Platnumz Atangaza Ratiba ya Ziara yake ya Marekani

[Picha: Diamond Platnumz Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Diamond Platnumz ametangaza kuwa kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu atakua kwenye ziara ya Marekani.

Tangazo la ziara hiyo inakuja wiki chache tu baada ya Diamond kugonga vichwa vya habari kutokana na mikutano aliyokuwa nayo na mastaa wa Marekani.

Soma Pia: Nandy Ajiunga na Kampuni ya Empawa Inayomilikiwa na Mr Eazi wa Ghana

Diamond kwa wakati huo alikutana na wadau mbali mbali katika tasnia ya burudani ya Marekani. Kulingana na ratiba aliyochapisha kwenye mtandao, ziara yake itaanza tarehe nane Oktoba na kukamilika tarehe 31 mwezi huo.

Aliorodhesha mikoa ambayo atatembelea katika ziara yake pamoja na tarehe ambazo atakuwa kwenye mikoa hiyo.

Kwa mfano, ataanza ziara yake akiwa mkoa wa Atlanta mnamo tarehe nane. Baada ya hapo, atakwenda Washington DC mnamo tarehe kumi kabla ya kuelekea Seattle tarehe kumi na tano.

Soma Pia: Hamisa Mobetto Atangaza Ujio wa Albamu Yake

Kisha atafika Minneopolis siku ifuatayo. Mikoa mingine ambayo Diamond atatua na kukutana na mashabiki wake ni pamoja na; New York, Louisville, Arizona, Houston, Boston na Dallas.

Ujumbe wa Diamond kuhusu ziara hio inatokea siku chache tu baada ya yeye kuwashauri wasanii wenzake kutoka bongo kuweza kuekeza katika kukuza na kuongeza mashabiki wao katika nchi za kigeni. Kulingana na Diamond, wasanii wengi wanahofia kufanya mambo mapya au kujaribu mitindo tofauti.

Leave your comment