Nandy Ajiunga na Kampuni ya Empawa Inayomilikiwa na Mr Eazi

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Nandy amejiunga na kampuni ya Empawa inayomilikiwa na msanii maarufu kutokea Nigeria Mr. Eazi.

Mr. Eazi katika chapisho alilolieka kwenye ukurasa wake wa Instagram alimkaribisha Nandy kwenye Empawa huku akimtambulisha rasmi kama mwanachama mpya wa kampuni hio.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Tano 5 Zinazotamba YouTube Tanzania Wiki Hii

Kando ya chapisho hilo, Mr. Eazi aliweka picha iliyomwonyesha akiwa na Nandy, na vilevile kuambatanisha picha ingine iliyooensha wimbo wa Nandy uitwao ‘Nimekuzoea’.

Kulingana na chapisho la Mr. Eazi, Empawa ilishiriki katika utengenezaji na usambazaji wa wimbo wa ‘Nimekuzoea’.

"Welcome @officialnandy to The emPawa Family & Big Congratulations!!! We Just Getting Started," Mr. Eazi aliandika mtandaoni.

Nandy wiki iliyopita alisafiri kwenda nchini Ghana ambako alikutana na Mr Eazi. Baadaye alichapisha picha iliyomwonyesha akiwa studioni pamoja na mtengenezaji wa muziki Producer Kimambo Beats. Chapisho la Nandy lilidhihirisha kuwa alikuwa amekwenda Ghana kwa kazi ya kimuziki.

Soma pia: Safari ya Nandy Kuelekea Ghana Yaibua Maswali

Kampuni ya Empawa si lebo ya kurekodi nyimbo kama vile wengi wanafikiria. Empawa inahusika katika usambazaji wa ngoma na pia kuongeza soko ya wasanii. Empawa hivyo basi inafanya kazi na wasanii wengi ikiwemo wale walio huru na wale waliosainiwa katiki lebo mbali mbali. Nandy kujiunga na kampuni hiyo ni mafanikio makubwa sana kwake Mr Eazi kwani Nandy ni mmoja wa wasanii wa kike wanaovuma si Tanzania tu bali Afrika Mashariki kwa jumla.

Leave your comment