Safari ya Nandy Kuelekea Ghana Yaibua Maswali

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki tajika kutoka Tanzania Nandy kwa sasa amesafiri kuelekea nchini Ghana. Malikia huyo wa muziki ya bongo aliwafahamisha mashabiki wake kuhusu safari yake kupitia ukurusa wake wa Instagram.

Kwenye chapisho hilo, Nandy alionekana akiwa ameabiri ndege. Msanii huyo hata hivyo hakufichua sababu kamili nyuma ya safari yake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Tano 5 Zinazotamba YouTube Tanzania Wiki Hii

Safari hio ya Nandy imeibua maswali mengi miongoni mwa wafuasii wake, huku wengine wakiuliza iwapo anaenda kufanya collabo na wasanii wa Ghana? Iwapo anaenda kutafuta wasanii wa kuwaalika kwenye tamasha lake la Nandy Festival, Iwapo anaenda kuwatumbuiza mashabiki wake uko ama ameenda kumalizia albamu yake inayotarajiwa baadaye mwakani.

Ni muhimu kutaja kuwa safari yake Nandy inakuja siku chache baada ya kufanikisha tamasha lake la Nandy festival kule Zanzibar.

Hapo nyuma, Nandy alisafiri kuelekea Nigeria na baadaye kumleta msanii Joeboy katika tamasha yake. Swali kuu kwa sasa limekuwa iwapo Nandy ataleta msanii wa Ghana kuja kutumbuiza katika tamasha yake ya Nandy.

Soma Pia: Nandy: Ilinigharimu Milioni 40 Kufanya Wimbo wa ‘Leo Leo na Koffi Olomide

Hivi karibuni pamekuwa na uhusiano wa karibu baina ya wasanii wa Tanzania na wale wa Afrika Magharibi. Wasanii wengi wa bongo wanaonekana kukimbilia Afrika Magharibu kwa minajili ya kupata kolabo. Baadhi ya wasanii waliochia kolabo na wasanii wa Afrika Magharibi ni Dayna Nyange ambaye alishirikiana na Davido.

Msanii mwingine ambaye amepota kolabo na mwamuziki wa Afrika Magharibi ni Zuchu ambaye alishirkiana na Joeboy. Nandy kwa sasa ni msanii anayevuma si Tanzania tu bali katika bara lote la Afrika. Anazidisha kukita mizizi kimuziki kupitia kolabo. Moja ya kolabo inayotarajiwa sana kutoka kwa Nandy ni wimbo wake na msani wa Afrika Kusini Sho Madjozi.

Leave your comment