Nandy: Ilinigharimu Milioni 40 Kufanya Wimbo wa ‘Leo Leo na Koffi Olomide

[Picha: Buzz Central]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka bongo Nandy ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Nimekuzoea’, ameweka wazi alitumia kitita kikubwa cha pesa katika wimbo wake wa ‘Leo Leo’ akimshirikisha Koffi Olomide.

Akifanya mahojiano na mtangazaji Lil Ommy, Nandy aliweka wazi kuwa ilimgharimu takribani Milioni 40 ili kuweza kufanya wimbo na wanamuziki Koffi Olomide kutokea Congo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: EP 5 Mpya Zilizoachiwa Bongo Mwezi Juni 2021

"Kumleta Koffi sio kitu kidogo imetumika zaidi ya Milioni 40 inaenda Milioni 50 na nilikuwa najua hiyo budget muda kwa hiyo kila tukipiga mahesabu acha niendelee kujichanga nikafikia hatua nikafanya," alisema msanii huyo.

Msanii huyo pia aliweka wazi kuwa yuko kwenye harakati ya kuandaa albamu mpya na kuwaomba mashabiki zake wampe muda wa kutosha wa maandalizi kwani kuandaa albamu sio kitu kidogo ila anatarajia, kuachia albam hiyo ndani ya mwaka huu.

"Ujue kufanya albamu sio kitu cha kitoto tunazungumzia nyimbo zaidi ya 10. Ni time energy na usiimbe imbe tu kwa hiyo tu wanipe time inshaaallah huu mwaka," alizungumza msanii huyo.

Tangu aanze muziki mwaka 2016 Nandy ametoa miradi kadhaa kwenye muziki wake ikiwemo albam ya "The African Princess" iliyotoka Novemba 9 mwaka 2018 albamu iliyofanya vizuri sana ndani na nje ya nchi.

Soma Pia: Nandy Atangaza Kolabo Mpya Na Sho Madjozi

Kuhusiana na kushindanishwa na Zuchu pamoja na wasanii wengine wa kike wa hapa nchini Tanzania Nandy aliweka wazi kwamba: "Na mimi naona ni kitu kizuri kwa sababu wanaona, kitu kizuri kwetu sisi sote na wanatupa morali ya kuona i have to work hard lakini wote tunapresent nchi yetu vizuri."

Aidha, Nandy alisema kuwa kama itatokea atahitajika kufanya kazi na msanii Zuchu kutokea WCB yeye hana hiyana ila inabidi mambo yaende kibiashara zaidi ili kila mtu afaidike

"As long as everything is okay, Yes. You know now mziki umekuwa kibiashara lazima ukifanya kitu kiwe kibiashara kwetu sisi sote. We are all brands, brands kubwa am pretty sure management yake itahitaji kuona kuna mafanikio, menejiment yangu itahitaji kuona kuna mafanikio," alidokeza msanii huyo.

Leave your comment