Nyimbo Mpya: EP 5 Mpya Zilizoachiwa Bongo Mwezi Juni 2021

[Picha: Dyana Nyange Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wakati wasanii kama Zuchu, Diamond Platnumz, Alikiba, Harmonize na Barnaba wanaposhangilia mwezi Juni kwa kutoa nyimbo kali ambazo zimependwa sana na watu. Kuna baadhi ya wasanii waliamua kuchukua njia tofauti kwa kuachia EP kwa mashabiki zao ili kuenda sawia na soko la muziki.

Soma Pia: Zuchu Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zilizomfanya Zuchu Kuwa Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki

Mwaka 2021 umepokea EP nyingi sana kutoka kwa wasanii wa Tanzania lakini zifuatazo ni EP ambazo zimetoka mwezi Juni mwaka huu.

Taste - Nandy

Mwanadada Nandy alifungua pazia la mwezi huu kwa kuachia EP yake ‘Taste’ yenye nyimbo nne ambazo ni ‘New Couple’, ‘Yuda’, ‘Yote sawa’ na ‘Nimekuzoea’. EP hio iliachiwa ili kusindikiza tamasha la Nandy Festival ambalo mpaka sasa limefanyika Kigoma, Mwanza, Dodoma na siku chache baadae linategemewa kurindima huko Arusha. Hii ni EP ya pili kwa Nandy ndani ya mwaka huu kwani mwezi aliachia EP ya nyimbo za dini inayojulikana kama ‘Wanibariki’.

Addicted – Ibrah Nation

Msahau kidogo Ibraah wa Konde Gang, msanii Ibrah Nation aliyeanzia muziki wake pale Tanzania House of Talent (THT) Juni 4 mwaka huu aliachia EP yake inayokwenda kwa jina la Addicted. EP ya Addicted imesheheni nyimbo 5 ambazo ni ‘Addicted’, ‘Salio’, ‘Mawenge’, ‘Tofauti’ pamoja na ‘Sina Muda’.  Ibraanation alikaririwa akisema EP yake ni tofauti na EP nyingine kwa kuwa ina mchanganyiko wa maudhui tofauti tofauti. "Kama ukifuatilia kwanzia wimbo wa kwanza mpaka wa mwisho kuna content tofauti, nilitaka pia nionyeshe uwezo wangu mwingine wa kuandika mashairi tofauti na mapenzi.," alisema msanii huyo.

Soma Pia: Dayna Nyange Afunguka Jinsi Alivyomshawishi Davido Kufanya Collabo Naye

Baba Bosi TV - Belle 9

EP hii kutoka kwa Belle 9 ilitoka tarehe 9 Juni na ina nyimbo 5 kama ‘Blue Tick’, ‘Without You’, ‘Freemason’, ‘Hayatabiriki’ pamoja na ‘On Fire’ aliyofanya na Rosa Ree. Kutokana na ubora wa EP hii Msanii Linex alisifia EP hii kwa kuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram: "EP ya Belle 9 ndio my best EP kwa sasa na iko kwa replay but my best song is Hayatabiriki. Go find good music."

Elo - Dayna Nyange

Dayna Nyange alitoa EP yake iliyosubiriwa kwa muda sasa inayoitwa ‘Elo’. Kitu kizuri kuhusiana na kazi hii ni kwamba Dayna ameimba nyimbo zote mwenyewe isipokuwa nyimbo ya ‘Elo’ tu aliyoshirikiana na msanii Davido kutokea nchini Nigeria. Ili kukuza mauzo ya EP hii, tarehe 28 May Dayna alishangaza watanzania kwa kuachia ya wimbo wake wa Elo na msanii Davido ambao mpaka sasa umetazmwa zaidi ya mara laki mbilii huko YouTube.

Carpricorn - Izzo Bizness

Mwanamuziki na mtangazaji wa kipindi cha On Air, Izzo business pia hakuwa nyuma kwenye suala la EP. Izzo B ambaye anaimba muziki wa Hip-hop aliachia EP yake mwezi huku akishirikiana na wasanii kama Mwasiti, Jaymoe, Ruth, Sugu pamoja na One six. EP ya Izzo bizness inakuja kipindi ambacho EP za wasanii wa Hip-hop zimekuwa chache sana hivyo basi msanii Izzo Bizness amekuja kuziba pengo hilo. Capricorn imesheni nyimbo 5 ambazo ni ‘Game ya bongo’, ‘Panda’, ‘Jessica’, ‘Umechange’ pamoja na ‘Ni Nani’.

Leave your comment