Nandy Atangaza Kolabo Mpya Na Sho Madjozi

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mashabiki wa Nandy wamejawa na furaha baada ya msanii huyo kutangaza kuwa hivi karibuni ataachia kazi mpya akimshirikisha msanii wa Afrika Kusini Sho Madjozi.

Nandy aliambatanisha ujumbe wake na video fupi iliyomwonyeshe akisakata densi pamoja na Sho Madjozi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Wimbo Mpya ‘Nimekuzoea’ Toka EP ya ‘Taste’

Wawili hao walikuwa wakicheza wimbo mpya wa Nandy ‘Nimekuzoea"’. Nandy ata hivyo, hakudokeza tarehe kamili ambayo kazi hiyo itaachiwa wala mada ya wimbo huo. Nandy alisema yeye pamoja na Sho Madjozi ni malkia ambao wanapenda nyimbo nzuri.

Msaniii huyo kwenye ujumbe wake alionekana mchangamfu sana huku akionyehsa kuwa kazi yake ijayo itakuwa ya kuburudisha sana.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Mpya za Zuchu, Nandy na Anjella Zinazovuma Bongo Wiki Hii

"Queens enjoying good music. @shomadjozi Africa they are not ready for us mamaaa," Nandy alisema.

Kwa sasa, Nandy ni mmoja wa wasani wa kike wanaotamba sana kwene tasnia ya burudani ya Tanzania. Hivi karibuni, Nandy amekuwa gumzo mtandaoni kutokana na mafanikio ya tamasha lake la Nandy Festival. Tamasha lijalo linatarajiwa kufanyika Zanzibar.

Sho Madjozi kwa upande mwingine anavuma sana Afrika Kusini. Madjozi ni msanii wa kipekee kwani ana mashabiki hadi Afrika Mashariki kutokana na uwezo wake wa kuongea lugha ya Kiswahili. Baada ya kujijengea jina nchini kwake nyumbani, Madjozi alifanya kolabo na wasanii wa bongo wakiwemo Marioo na Darassa.

Nandy na Sho Madjozi wanajulikana kwa kutoa nyimbo za kasi na tena za kuburudisha. Je wimbo unaotarajiwa kutoka kwa wasanii hawa wawili utakuwa wa kunengua viuno ama wa mahaba? Muda tu ndio utabaini ukweli.

Leave your comment