Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Wimbo Mpya ‘Nimekuzoea’ Toka EP ya ‘Taste’

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Nandy ameachia wimbo moya kwa jina ‘Nimekuzoea’.

‘Nimekuzoea’ ni ngoma ya kwanza kutoka kwenye EP yake mpya yenye jina ‘Taste’.

Soma Pia: Nandy Festival: Alikiba, Marioo na Baba Levo Kuongoza Tamasha Wikendi Hii

"Nimekuzoe" ni wimbo wa mapenzi ambao unasimulia hadithi ya msichana mchanga ambaye yuko kwenye mapenzi na mraibu wa mwenzake.

Unaposikiza ngoma hii, unahisi uzito na mhemko katika sauti ya Nandy anapoelezea hisia zake kwenye wimbo. Nandy amebarikiwa sana na ana uwezo wa kumfanya msikilizaji wake ahusiane na hali ya wimbo.

Kimambo Beats ndiye aliyetengeza ngoma hii, ingawa mdundo umebadilika kidogo kutoka kwa nyimbo zake za awali. Wimbo huu una kasi ambayo ni ya kutosha kumfanya msikilizaji kunengua kiuno.

‘Nimekuzoea’ imepokelewa vizuri na inawatazamaji zaidi ya elefu arobaini kweneye mtandao wa YouTube.

Kanda ya ngoma hii bado haijaachiliwa lakini inatarajiwa hivi karibuni.

Soma Pia: Wasifu wa Nandy, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Kwingineko, Nandy anatarajiwa kuachia nyimbo zingine kwenye EP hio siku zijazo.  Nandy kwa sasa yuko Kigoma pamoja na timu yake ya wanamuziki watakaoburudisha mashabiki kwenye tamasha ya nandy Festival.

Tamasha hio itafanya wikendi hii na inawajumuisha wasanii wengi tajika kama vile; Marioo, Alikiba, Baba Levo na wengine wengi.

https://www.youtube.com/watch?v=QX3aG3FJ49g

Leave your comment