Nandy Festival: Alikiba, Marioo na Baba Levo Kuongoza Tamasha Wikendi Hii

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nandy pamoja na timu yake wanatarajiwa kuwasili Kigoma Ijumaa kwa matayarisho ya Nandy Festival ambayo itafanyika Jumamosi.

Nandy amesaini baadhi ya wanamuziki bora nchini Tanzania kutumbuiza katika hafla hiyo.

Soma Pia: Wasifu wa Nandy, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Wanamuziki watakaowaburudisha mashabiki kwenye tamasha la Nandy ni pamoja na Babalevo, Mario, Mabantu, Stamina, Whozu miongoni mwa wengine.

Alikiba alithibitisha uwepo wake kwenye tamasha la Nandy ambapo pia atatarajiwa kutumbuiza.

Alikiba katika uthibitisho wake aliwasihi Watanzania kuwaunga mkono waimbaji wa kike. Alikiba alieleza kuwa anapenda bidii na kujitolea ambayo Nandy alikuwa amewekeza katika kazi yake na ndio sababu alikuwa amejitokeza kumuunga mkono.

Soma Pia: Zuchu vs Nandy: Ni nani Bora Zaidi?

"Sanaa yetu ina upungufu wa wasanii wa kike, inabidi waliopo wapewe nguvu ill waweze kufanikiwa zaidi. @officialnandy ni msanii anayejituma na mwenye jitihada. Napenda anachofanya na ndio maana Jumamosi ijayo nitaenda nyumbani Kigoma kumpa support katika #NandyFestival," Alikiba alisema.

Nandy amesifiwa na wadau mbali mbali katika tasnia ya burudani ya Tanzania kwa weledi na kujitolea ambayo ameonyesha katika kujiandaa na tamasha la Nandy 2021.

Nandy hufanya tamasha hili kila mwaka ambapo huleta wasanii wa juu pamoja kuwaburudisha mashabiki. Nandy amehusisha walindausalama katika maandalizi yake na usalama unatarajiwa kuwa juu katika hafla hiyo.

Leave your comment