Wasifu wa Nandy, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nandy ni nani na ana miaka mingapi?

Jina la usani: Nandy

Jina Halisi: Faustina Charles Mfinanga

Tarehe ya kuzaliwa: Novemba 9, 1992 (miaka 29)

Aina ya mziki: Bongo Fleva

Thamani ya jumla: Inakisiwa kuwa dola milioni moja hadi milioni tano

Nandy alizaliwa mnamo Novemba 9, 1992 mjini Moshi, Tanzania. Alisomea shule ya Msingi ya Julius Nyerere, kisha baadae alijiunga na shule ya Upili ya Lomwe na hatimiya alienda Chuo cha Elimu ya Biashara cha CBE.

Nandy alianzaje kazi ya usanii?

Nandy alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 6. Alipoingiza miaka 15, alijiunga na kwaya ya shule, hatua ambayo ilimsaidia kuboresha umahiri wake wa kuimba. Baadaye, aliyekuwa mwendani wake Ruge Mutahaba, Mtendaji Mkuu wa Tanzania House of Talent (THT) alimchukua katika hema lake la sanaa.

Wakati wake huko THT, alikutana na Emma the Boy ambaye alifanya kazi naye kwenye wimbo wake wa kwanza wa 'Nagusagusa' mnamo mwaka 2016. Awali mwaka 2015, Nandy alijiunga katika tamasha ya Tecno Own the Stage nchini Nigeria na aliibuka katika nafasi ya pili. Kufuatia mashindano hayo, Nandy alianza kupata uzoefu kimuziki, aliohitaji katika kupiga hatua katika mziki wake.

Mnamo 2017, aliachia wimbo wake maarufu wa “One Day” ambao ulitamba sana na hata kumpa fursa ya kuwa miongoni mwa wasanii walioshiriki Coke Studio Africa mnamo 2017. Baada ya hapo, Nandy alianza kutoa ngoma moja baada ya nyingine, na kwa sasa ni mmoja wa wanamuziki tajika nchini Tanzania.

Baadhi ya nyimbo zake bora ni pamoja na

  • Nguvu
  • Leo
  • Number One
  • Siku Moja
  • Acha Lizame
  • Ninogeshe
  • Kiza Kinene
  • Kongoro
  • Subalkheri
  • Baikoko
  • Nigande
  • Bado

Nandy ana Tuzo Ngapi?

Nandy ameshinda tuzo kadhaa zikiwemo; Msanii bora wa Kike Afrika Mashariki kwenye Tuzo za All Africa Music 2017 Mgeni bora wa Kike kwenye Tuzo za AMI Africa, Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki Kwenye Tuzo za AFRIMA 2020.

Maisha Ya Nandy Nje Ya Muziki

Mbali na muziki, yeye ni mpenda mitindo na ndiye mmiliki wa Prints by Nandy Africa. Yeye pia ni balozi wa UNICEF, mwanamitindo wa nguo za harusi za kina dada na miliki wa Make up by Nandy.

Soma Pia: Zuchu vs Nandy: Ni nani Bora Zaidi?

Nandy ana uhusiano na nani?

Mwaka wa 2020, mwimbaji huyo alipewa pete na Billnass na kwa sasa wanachumbiana.

Leave your comment