Hamisa Mobetto Atangaza Ujio wa Albamu Yake

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarafu nchini Tanzania Hamisa Mobeto ametangaza kuachia yake albamu yake mwishoni mwa mwaka huu. Mobetto amesema hayo kwenye kipindi cha XXL kinachoruka Clouds FM.

Katika mahojiano hayo, Hamisa alisema kuwa iwapo mipango yake itaenda sawia kama anavyotaka, basi mwishoni mwa mwaka huu anaweza kuachia albamu yake ya kwanza tangu aanze muziki.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Kuachia Wimbo Mpya Wenye Jina ‘Mang'dakiwe’ Remix Wiki Hii

"Kama mipango itaenda sawa kama ninavyotarajia probably mpaka mwisho wa mwaka album itakuwa tayari ishatoka," alidokeza mwanamuziki huyo.

Kutokana na tangazo hilo, Mobetto anaungana na wasanii wengine kama Harmonize, Diamond Platnumz, Alikiba, Marioo, Whozu, Ibraah, Country Boy, Anjella na Kili ambao wametangaza kuwa wako mbioni kuachia albamu.

Soma Pia: Nandy Afichua Sababu Kuu Iliyompeleka Ghana

Aidha kupitia mahojiano hayo, Mobetto aliweka wazi kuwa amefurahishwa na mapokezi ya wimbo wake wa ‘Ex Wangu’ remix aliofanya na Seneta Kilaka.

"Ni mara yangu ya kwanza kuimba nyimbo ya Singeli watu wameipokea vizuri sana, sio watu tu watanzania mpaka nje ya nchi ya Tanzania. Kwa hiyo nina furaha sana sijutii na ninaona ni maamuzi sahihi niloyachagua kufanya hii nyimbo," alisema Mobetto.

Bila shaka, mafanikio ya wimbo wa ‘Ex Wangu’ Remix" yanaonekana dhahiri shahiri kwani kufikia sasa video ya wimbo hio iliyotoka Julai 9 imetazamwa mara milioni mbili nukta nne kwenye mtandao wa YouTube na umekaa takribani wiki tatu mfululizo kwenye video zinazotamba kwenye mtandao huo.

Leave your comment