Harmonize Atangaza Kuachia Wimbo Mpya Wenye Jina ‘Mang'dakiwe’ Remix Wiki Hii

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Harmonize ametangaza kuwa wimbo wake wa ‘Mang'dakiwe’ remix utaachiwa muda wowote wiki hii. Katika taarifa aliyochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alieleza kuwa tayari utengenezaji wa ngoma hiyo ushakamilika na ilichosalia tu ni kuiachia.

Harmonize hata hivyo hakutoa siku kamili ambayo atadondosha wimbo huo. Aliwauliza mashabaki wake kutoa maoni yao kuhusu siku wangependa ngoma hiyo ichapishwe mtandaoni.

Soma Pia: Nyimbo Mpya:Ngoma 5 Zilizoachiwa Bongo na Rayvanny, Marioo na Barakah the Prince

Aidha, Harmonize aliahidi kuwa atampea shabiki wake mmoja shilingi milioni moja iwapo ataweza kutoa wakati wa kuchapisha video hiyo na pia kushawishi uongozi wake.

"The movie is ready and we are dropping this week niambie ungependa uione lini na sangapi ukiweza kutoa muda & siku sahihi ukaishawishi managment nzima..!!! utajishindia kamilioniiiii ka moja masikini na masikini mwenzie ....!!! haya pendekeza na ushinde," Harmonize aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

Soma Pia: Madai ya Ununuzi wa Watazamaji Yaibuka Baada ya Diamond, Alikiba Kuachia Nyimbo Zikifuatana

Tangazo hili liliwasisimua mashabiki wake ambao walikuwa wamesubiri kwa hamu sana wimbo huo. Hapo awali,Harmonize alikuwa ametangaza kuwa yuko studuio pamoja na msanii wa Afrika Kusini Dj Obza.

Ngoma hiyo ya ‘Mang'dakiwe’ remix inatarajiwa kuwa kubwa sana kwa sababu ngoma halisi ilipata mamilioni ya watazamaji katika mtandao wa YouTube. Ushirikisho wa msanii wa Afrika Kusini pia itachangia pakubwa katika mafanikio ya ngoma hiyo.

Kwa sasa wasanii wa bongo wameinga katika mtindo wa kufanya ngoma wakitumia midundo za Amapiano kuto Afrika Kusini.

Leave your comment