Madai ya Ununuzi wa Watazamaji Yaibuka Baada ya Diamond, Alikiba Kuachia Nyimbo Zikifuatana

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Madai kuwa kuna wasanii wa Bongo wanao nunua watazamaji kwenye mtandao wa YouTube yameibuka tena baada ya wasanii Diamond Platnumz na Alikiba kaucha ngoma za mpya zikifuatana.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba Aachia Video ya ‘Jealous’ Akimshirikisha Mayorkun

Wiki iliyopita, Diamond aliachia video ya ‘Iyo’ na siku moja baadaye, Alikiba akaachia ‘video ya ‘Jealous. Video ya Alikiba ya ‘Jealous’ ilivuma sana mtandaoni na kuipiku ile ya Diamond ya wimbo wa ‘Iyo’.

Video yake Alikiba ilipata watazamaji milioni moja ndani ya masaa kumi na mbili huku ya Diamond ikipata idadi sawia ndani ya masaa kumi na tatu.

Diamond baadaye alichapisha ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram ambapo alikisiwa kumtupia dongo Alikiba kuhusu ununuzi watazamaji, japo hakumtaja jina.

Soma Pia: Yogo Beats Afunguka Kufanya Kazi na RudeBoy Kwenye ‘Salute’ya Alikiba

"Real Definition of a Hit na wimbo pendwa....Ubaya wa vyakununua Haupati vitu kama hivi," chapisho la Diamond lilisoma.

Timu ya Alikiba kupitia ukurasa wa Instagram wa Kings Music Records walichapisha ujumbe baadae uliosema kuwa lilikuwa jambo la kushangaza kuwa wanopenda idadi kubwa ya watazamaji kwa sasa wanakashifu.

 "Wapenda namba leo hawazitaki, wamepaniki. Dozi itaendelea vumilieni -mFeel the music, enjoy it and Don’t get Jealous," ujumbe kutoka Kings Music ulisoma.

Alikiba pia kibinafsi kupitia ukurasa wake wa Instagram vile vile aliandika chapisho lilisoma "Don't get Jealous" muda mfupi baada ya Diamond kuweka chapisho lake.

Leave your comment