Nyimbo Mpya: Alikiba Aachia Video ya ‘Jealous’ Akimshirikisha Mayorkun

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Alikiba kutoka lebo ya Kings Music ameachia video ya wimbo wake wa ‘Jealous’ akimshirikisha Mayorkun kutokea nchini Nigeria.

‘Jealous’ imesheheni uigizaji mahiri na stori nzuri ambayo inaendana kabisa na maudhui ya wimbo. Kwenye sehemu ya kwanza ya video, Kiba anaonekana akiwa kwenye mandari (picnic) na mpenziwe ambaye anaonekana ana wivu sana. Kiba anatumia aya ya kwanza kwenye wimbo kumtuliza.

Soma Pia: Babalevo Asisimua Mashabiki kwa Kusifia Ngoma Mpya Ya Alikiba 'Jealous'

Mayorkun anaonekana kutawala sana kwenye sehemu ya pili ya video akiwa na Alikiba kwenye casino wakionekana kucheza kamari. Kulingana na stori ya video, wanaimba na kucheza wakiwahasa wapenzi waliokuwa nao hapo kwenye casino wapunguze wivu.

Video ya ‘Jealous’ imefanyika nchini Nigeria chini ya uangalizi mkubwa wa director wa kike aitwaye Dayamund anayefanya kazi chini ya kampuni ya Pink Line Films, kando na video hii Dayamund ameshafanya kazi na wasanii wakubwa kutokea Nigeria kama Chike kwenye video ya "If you no love" mwishoni mwa mwaka jana.

Soma Pia: Alikiba Aeleza Sababu ya Kuchelewa Kwa Albamu Yake

Kufikia sasa, video ya ‘Jealous’ imeshatazamwa mara 48,000 kwenye mtandao wa YouTube.

Kwa mwaka huu, hii ni video ya nne kutoka kwa Alikiba nyinginezo ni kama vile ‘Infedele’, ‘Ndombolo’ na ‘Salute’.  Alikiba amekuwa anatoa ngoma mfululizo kama sehemu ya maandalizi ya albamU yake ya tatu ambayo iko mbioni kutoka.

https://www.youtube.com/watch?v=LQyCY1t--GU

Leave your comment