Babalevo Asisimua Mashabiki kwa Kusifia Ngoma Mpya Ya Alikiba 'Jealous'

[Picha: Babalevo Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa Bongo Babalevo amewashangaza watumiaji wa mitandao ya kijamii baada ya kujitokeza na kumpongeza Alikiba kwa kuachia ngoma ya Jealous. Babalevo aliandika chapisho katika ukurasa wake wa Instagram ambapo alisifu wimbo wa Alikiba.

Soma pia: Nyimbo Mpya: Alikiba, Mayorkun Waachia Wimbo Mpya 'Jealous'

Sababu kuu ya chapisho hilo kuwaacha wengi wakiduwaa ni kuwa Babalevo amejulikana kwa kuwa mfuasi sugu wa Diamond Platnumz. Ufuasi wake kwa Diamond ulimfanya kuwa mkosaji mkuu wa wasanii woe ambao walikua wapinzani wa bosi huyo wa WCB.


Hivyo basi siku zote Babalevo amejilukana kuwa upande tofauti na Alikiba katika masuala ya kimuziki.

"GOOD MUSIC LINK KWA KING KIBA," Babalevo aliandika mtandaoni.

Pongezi la Babalevo lilipokelewa na hisia tofauti miongoni mwa wafuasi wake katika mitandao wa kijamii. Wengi walibaki na maswali chungu nzima kuhusu ni kipi kilimpa Babalevo msukumo wa kumsifia Alikiba kwa mara a kwanza katika historia y Bongo Flava.

Ufuasi sugu wa Babalevo kwa Diamond umefanya yeye kubandikwa jina la chawa wa WCB. Babalevo kwa upande wake hajawahi kubaili ufuasi wake kwa Simba na siku zote husimama kidete na kumtetea Diamond.

Mnamo tarehe 21 mwezi Julai Alikiba alitoa wimbo wa Jealous akimshiikisha Mayorkn. Wimbo huo umepokelewa vizuri na mashabiki na kupata zaidi ya wafuasi nusu milioni ndani ya siku mbili. Kwa sasa mashabiki wanasubiri kwa hamu sana kutazama video ya ngoma hiyo. Alikiba bado hajatangaza siku ya kuachia video.

Leave your comment