Nyimbo Mpya: Alikiba, Mayorkun Waachia Wimbo Mpya 'Jealous'

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki na mkurugenzi mtendaji wa Kings Music, Alikiba ameendelea kutimiza ahadi yake ya kuachia ngoma "back to back" baada ya kutoa wimbo mpya uitwao "Jealous" ambao amemshrikisha msanii kutokea Nigeria Mayorkun.

Soma Pia: Video 5 Zilizo na Watazamaji Wengi Zaidi YouTube Tanzania

Wimbo wa "Jealous" umetayarishwa na kufanyiwa maandalizi ya mwisho na Yogo Beats ambaye pia amehusika kutayarisha nyimbo kadhaa za Alikiba kama "Infedele" pamoja na "Salute". 

"Jealous" ni wimbo wa mapenzi na kwenye wimbo huu Alikiba ameendelea kuonyesha ufundi wake kwenye uandishi wa nyimbo  hizo kwani kwenye wimbo huu Alikiba anamthibitishia mpenzi wake kuwa anampenda na kumthamini hivyo asione wivu. 

Kwenye aya ya kwanza ya wimbo huu Alikiba anaimba : 

"We ndo my pain killer kushinda hata panadol umejaa mapenzi mashetani wanakaa kando, Oooh Shushu you for me, from Zero to Hero, bado tuko pamoja why you getting jealous?" 

Kwenye aya ya pili anaingia msanii Mayorkun ambaye anazidi kunogesha kibao hiki kwa kuimba kiingereza chenye lafudhi ya Nigeria." Plenty girls on my matter but i no dey shake cassava. Girl I'm for you only you. I'm trying to please you now, you still getting jealous?" 

Alikiba kumshirikisha Mayorkun kwenye wimbo huu kunamfanya Kiba awe msanii wa pili kutokea Tanzania kufanya kazi na Mayorkun ambaye yuko chini ya usimamizi wa Davido, Rayvanny alimshirikisha msanii huyu mwenye miaka 27 kwenye" Gimmi Dat" wimbo uliotoka mwaka 2019 na kufanya vizuri sana. 

Mashabiki wameonekana kupenda na kufurahi kazi hii mpya ya Alikiba kwani wengi wao kupitia akaunti ya Youtube ya Alikiba wametoa maoni chanya kuhusu wimbo huu 

Mmoja wa wachangiaji aliandika "When two great artists come together. King Kiba never disappoints" 

Mchangiaji mwingine alimpongeza Alikiba kwa kufanya muziki mzuri aliandika "Alikiba ukimya wake ulikuwa na siri kubwa ndani yake, King Kiba kweli unafanya muziki" 

Wiki chache zilizopita Kiba aliweka wazi kuwa mpaka pale albam yake inayosubiriwa kwa hamu sana na mashabiki zake itapotoka, atakuwa anatoa nyimbo mfululizo kama sehemu ya maandalizi ya kuachia albam. 

Pamoja na kukosa video lakini Audio ya wimbo huu imeshasikilizwa takriban mara, 74,000 kwenye mtandao wa Youtube ndani ya muda mfupi tu. 

https://www.youtube.com/watch?v=S1DQA8peH7M&ab_channel=Alikiba

Leave your comment