Video 5 Zilizo na Watazamaji Wengi Zaidi YouTube Tanzania

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii wa Tanzania hutegema sana mtandao wa YouTube kama kimbilio lao linapokuja suala la kuweka kazi zao hasa video za muziki. Utamaduni huu ulianza mwanzoni mwa miaka ya 2010 pale ambapo mtandao wa YouTube ulianza kuwa maarufu hapa Tanzania.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond Aachia ‘Iyo’ Akiwashirikisha Focalistic, Mapara A Jazz na Ntoshi Gazz

Makala hii inaangazia video tano za muziki kutoka Tanzania ambazo zimetazamwa sana kwenye mtandao wa YouTube kwa muda wote.

Soma Pia: Harmonize Awapongeza Nandy, Hamisa Mobetto na Anjella Kwa Kuachia Ngoma Zinazovuma

Yope remix - Innos B ft Diamond Platnumz

Video ya wimbo huu ilitoka Septemba 7 mwaka 2019 na kufikia sasa imetazamwa mara Milioni mia moja hamsini na tisa. Hii ndio video pekee iliyofanywa na msanii wa kitanzania ambayo imevuka watazamaji Milioni 100 kwenye mtandao wa Youtube.

https://www.youtube.com/watch?v=ebZ7Ng1okCg

Inama - Diamond Platnumz ft Fally Ipupa

Muunganiko wa Afro-Congo na Bongo Flava ulifanya video ya ‘Inama’ iweze kunoga sana. Video hii iliachiwa rasmi Juni 9 mwaka 2019 na kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni tisini na tatu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=x96N7f62GE4

Kwangwaru - Harmonize ft Diamond Platnumz

Video ya ‘Kwangwaru’ ilitoka April 14 mwaka 2018. Harmonize aliweka wazi kuwa ‘Kwangwaru’ ilikuwa na lengo la kuonesha kuwa muziki wa Bongo Fleva unaweza ukafanya vizuri hata kwenye kumbi za starehe kama klabu. Kufikia sasa video hii imeshatazamwa takriban mara Milioni themanini na tatu.

https://www.youtube.com/watch?v=0Wbc5ZwkAMw

Waah - Diamond ft Koffi Olomide

Novemba 30 mwaka 2020 ndio wimbo huu ulitoka na video yake alifanya Director Kenny kutokea Zoom Extra. Video hii iliweza kuvunja rekodi tofauti tofauti kama kufikisha watazamaji milioni 1 ndani ya saa nane na kufikisha watazamaji milioni 10 ndani ya siku saba na kufikia sasa video imetazamwa takriban mara Milioni sabini na saba kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=HCuTwNgY3_M

Nana - Diamond Platnumz ft Mr Flavor

Mwaka 2015 Mei 29 ndio siku ambayo Diamond Platnumz alitoa video ya wimbo wa Nana akimshirikisha Flavour kutokea nchini Nigeria. Wimbo huu ulipata mafanikio makubwa kiasi cha kumfanya Diamond Platnumz kuitwa kutumbuiza kwenye tuzo za MTV Africa Music Awards Durban Afrika Kusini. Kufikia sasa, video ya wimbo huu iliyoongozwa na Godfather Productions kutokea Afrika kusini imetazamwa mara Milioni sabini nne kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=IflpfcHmq5I

Leave your comment