Alikiba Aeleza Sababu ya Kuchelewa Kwa Albamu Yake

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Bongo Alikiba amefunguka sababu za kucheleweshwa kwa albamu yake. Alikiba wakati akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, alifafanua kuwa nyimbo alizotoa hivi karibuni zitakuwa kwenye albamu yake inayokuja.

Alikiba alisema kuwa alikuwa amepanga kuachia albamu hiyo mapema lakini ilibidi aicheleweshe kwa sababu ya shughuli za kuifanya matayrisho ya mwisho. Walakini, aliripoti kuwa albamu hiyo ilikuwa katika hatua za mwisho.

"Hizo ni nyimbo ambazo nimezi introduce tu lakini zitakuwepo kwenye album vile vile. Album inatoka anytime from now. Kuna vitu zenye zime delay tu dakika za mwisho kwa sababu za mastering na nini. Soon hiyo album inatoka," Alikiba alisema.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba, Rudeboy Waachia Wimbo Mpya 'Salute'

Hivi karibuni Alikiba aliachia wimbo uliopewa jina ‘Ndombolo’ ambao alishirikiana na wanamuziki kutoka kwa lebo yake ya rekodi King's Music. Wimbo huo umefanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube na kupata mamilioni ya watazamaji.

Alikiba ni mmoja wa wanamuziki bora nchini Tanzania ambao wanatarajiwa kuachia albamu zao mwaka huu. Wengine ni kama vile; Diamond Platnumz, Harmonize miongoni mwa wengine.

Soma Pia: Alikiba ft K2ga, Abdukiba and Tommy Flavour ‘Ndombolo’: New Music Tanzania [Official Video]

Leave your comment