Nyimbo Mpya: Alikiba, Rudeboy Waachia Wimbo Mpya 'Salute'

[Picha: More Exclusive]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Tanzania Alikiba ameshirikiana na mwimbaji nyota wa Nigeria Rudeboy katika wimbo wake mpya unaoitwa 'Salute'.

‘Salute’ ni wimbo unaoangazia changamoto ambazo Alikiba na Rudeboy wamepitia katika maisha yao ya ndoa.

Soma Pia:Alikiba, Abdukiba, K2ga na Tommy Flavour ‘Ndombolo’: Nyimbo Mpya Tanzania 

Wawili hao wanatoa shukrani kwa wake zao ambao walibaki waaminifu licha ya changamoto za kimaisha ambazo walipitia kutokana na umasikini.

Alikiba na Rudeboy aidha wanaahidi kubaki waaminifu kwa wapenzi wao na kufurahiya matunda ya mapenzi pamoja.

Soma Pia: LYRICS: Alikiba - Ndombolo ft. Abdu Kiba, K2ga and Tommy Flavour (Download)

"You got baby Face. Your dimples and eyes, Am lost in you Girl, Oh yeah yeah, Mtihani liite testii, Ila umegandana nami all along, Ahh Oh yeah yeah, Nilipochoka we ndo stamina, Faraja hata kwa shida yeah, That time nilikuwa sina, Now tu enjoy nawe," Alikiba aliimba.

‘Salute imepokelewa vizuri na ina zaidi ya watazamaji laki moja masaa chache baada ya kuachiwa. Kwa sasa, kanda ya ngoma hio bado haijachiwa, lakini ripotizinaeleza kuwa itatolewa hivi karibuni.

Alikiba ni mmoja wa wanamuziki wanaoongoza Afrika Mashariki wakati Rude Boy pia ni miongoni mwa wanamuziki maarufu kutoka Afrika Magharibi. Ushirikiano huo ni njia ya kuleta mikoa miwili pamoja.

https://www.youtube.com/watch?v=XOsaB1HbB6s

Leave your comment