Alikiba, Abdukiba, K2ga na Tommy Flavour ‘Ndombolo’: Nyimbo Mpya Tanzania

[Picha: Kings Music Instagram]

Mwandishi: Omondi Otieno

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi Mkuu wa Kings Music Tanzania Alikiba ameachia ngoma mpya kwa jina ‘Ndombolo’ akiwashirikisha Abdukiba, K2ga na Tommy Flavour.

‘Ndombolo’ ni wimbo wa kisasa unaonangazia densi halisi ya Kiafrika ‘Ndombolo’ kutoka maeneo ya Congo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu, Diamond, Alikiba na Wasanii Wengine Wanoatarajiwa Kuachia Ngoma Mpya

Wimbo huu umetengezwa na una mdundo wa kusisumua san asana kwa wanaopenda densi.

Akizungumza baada ya kuachia ngoma hii, Alikiba amesema kuwa ataanza kuachia nyimbo mpya zikifuatana hadi atakapokuwa tayari kuachia albamu yake baadaye mwakani.

“Summer is here and it’s going to be fun, Dropping music Back 2 Back until my Album is Out !! New Song with my Kings Music Family,” Alikiba aliandika kwenye Instagram.

Soma Pia: Zuchu Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zilizomfanya Zuchu Kuwa Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki

Kwa sasa, kanda ya wimbo huu bado haijachiwa, lakini inakisiwa kuwa itatoka hivi karibuni.

‘Ndombolo’ imepokelewa vizuri na inawatazamaji zaidi ya elefu sitini kwenye YouTube masaa chache baada ya kuachiwa.

Hii ndiyo kazi ya kwanza iliyowaleta pamoja wasanii hao wa Kings Music mwaka huu.

Kwingineko, Watanzania bado wanasubiri wimbo wa kipekee kutoka kwa Alikiba, kwani amekua akifanya kazi za kushirikiana, lakini bado hajaachia ngoma pekee yake.

https://www.youtube.com/watch?v=VkIlQNegH7k

Leave your comment