Yogo Beats Afunguka Kufanya Kazi na RudeBoy Kwenye ‘Salute’ya Alikiba

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtayarishaji wa muziki kutokea nchini Tanzania Yogo Beats ameelezea ni kwa namna gani aliweza kufanya kazi na msanii RudeBoy kutokea Nigeria kwenye ‘Salute’ ya Alikiba.

Yogo Beats ameeleza hayo akiwa anafanya mahojiano kwenye kipindi cha The Switch ambapo ameweka bayana kuwa alitengeneza mdundo wa wimbo huo akiwa na msaidizi wake aitwaye Al Kiz na baada ya kutengeneza walitumiwa wasanii kadhaa ambao hakutaka kuwataja majina ili waingize sauti lakini walichelewa kuleta majibu.

Soma Pia:Babalevo Asisimua Mashabiki kwa Kusifia Ngoma Mpya Ya Alikiba 'Jealous' 

"Beat tulianza kufanya mimi na kijana wangu ambaye nafanya nae kazi anaitwa Al Kiz before Alikiba kuja na baadae wimbo uliandaliwa vizuri na ukatumwa kwa baadhi ya wasanii wawili watatu hivi ubaya ni kwamba walichelewa kurudisha majibu kwa wakati so by the time tuko South Africa ikaja option ya kumtumia RudeBoy," alidokeza nguli huyo wa muziki.

Yogo Beats alifafanua kuwa RudeBoy alipopewa wimbo huo aliupenda sana na akakubali kurekodi mara moja kisha Yogo na Alikiba walipopata safari ya kwenda Nigeria ndipo walipopata wasaa wa kukamilisha kila kitu.

"Tukarudi Tanzania tukakaa kwa muda fulani tukapata safari ya kulekea Nigeria, tulivyofika Nigeria tukakutana na RudeBoy tukarekodi tena Verse,” alisema producer huyo.

 Kando na ‘Salute’, Yogo Beats amehusika kutayarisha nyimbo mbalimbali za Alikba kama ‘Infedele’, ‘Mediocre’ na hata wimbo wa ‘Nibakishie’ ambao Alikiba ameshirikishwa na mwanadada Nandy.

Soma Pia: Alikiba Asifia Ustadi wa Diamond Katika Kutunga Wimbo wa 'Kamata'

Kufikia sasa, video ya wimbo wa ‘Salute’ imetazamwa mara Milioni 4 nukta tano kwenye mtandao wa YouTube ndani ya mwezi mmoja tu.

Leave your comment