Alikiba Asifia Ustadi wa Diamond Katika Kutunga Wimbo wa 'Kamata'

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kando na kuwa wasanii wenye ushawishi mkubwa sana katika tasnia ya muziki ya Tanzania, Alikiba na Diamond Platnumz pia ni wapinzani wenye historia ndefu sana. Uhasama baina ya wasanii hawa wawili tajika haukuanza jana, bali enzi ya zamani ya Bongo Flava.

Wawili hao wamekuwa maji na mafuta licha ya baadhi ya wadau mbali mbali kujaribu kuwaleta pamoja. Hivyo basi lilikuwa jambo la kufurahiha sana haswaa kwa mashabiki pale Alikiba alifunguka na kusifia ustadi wa Diamond katika kutunga nyimbo za burudani.

Alikiba alipokuwa katika mahojiano kwenye kituo cha redio, aliulizwa atoe kauli yake kuhusu mtindo wa uradidi ulioshuhudiwa katika wimbo wa Kamata ulioimbwa na Diamond. Mtindo huo wa Diamond kurudia neno moja mara mingi katika wimbo umekuwa mjadala mkubwa haswaa baina ya watunzi wa mashairi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba, Mayorkun Waachia Wimbo Mpya 'Jealous'

Alikiba kwa upande wake alisema kuwa mtindo huo ni wa kuburudisha na mashabiki wanaufurahia sana. Msanii huyo ambaye pa ni mkurugenzi mkuu wa King's Music alifafanua kuwa hapakuwepo na maana fiche katika mtindo huo pasi na kutoa burudani.

"Utunzi huo kiukweli mimi naona kwamba ni kuburudisha tu. Ni kuburudisha tu wala hakukuwa na maana yeyote. Lakini imependeza," Alikiba alieleza.

Soma Pia: Babalevo Asisimua Mashabiki kwa Kusifia Ngoma Mpya Ya Alikiba 'Jealous'

Mashabiki wamemsifia sana Alikiba kwa kuonyesha busara katika majibu yake. Alikiba kwa sasa yupo katika harakati ya kuunda albamu yake. Kwa sasa anazidi kuachia nyimbo mfululizo. Wimbo aliochia hivi karibu umepewa jina la ‘Jealous’.

Leave your comment