Nandy Afichua Sababu Kuu Iliyompeleka Ghana

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wiki iliyopita msanii Nandy alisafiri kuelekea nchini Ghana. Safari yake iliibua maswali mengi kwani Nandy hakuwa ameelezea kilichompeleka Ghana.

Soma Pia: Nandy: Ilinigharimu Milioni 40 Kufanya Wimbo wa ‘Leo Leo na Koffi Olomide

Nandy hata hivyo hatimaye amefichua sababu kuu nyuma ya safari yake. Kupitia mtandao wa Instagram, Nandy alieleza kuwa alisafiri Ghana kwa kazi ya kimuziki. Aliyemkaribisha nchini Ghana alkua msanii tajika Mr Eazi.

Kulingana na taarifa ambayo Nandy alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram inaonekana kuwa alienda Ghana kurekodi wimbo. Kwenye picha moja aliyochapisha, Nandy alionekana akiwa studio na mtayarishaji wa midundo Kimambo Beats.

Yaonekana kuwa Nandy yupo katika harakati ya kufanya kazi na wasanii mbali mbali wa Afrika. Hapo awali Nandy alitangaza kuwa alikuwa studioni na msanii wa Afrika Kusini Sho Madjozi kwa sababu ya kurekodi kolabo.

Soma Pia: Nandy Atangaza Kolabo Mpya Na Sho Madjozi

Aliambatanisha ujumbe huo na video iliyomwonyesha akisakata densi pamoja na Sho Madjozi.

Mashabiki wengi wanasuburi kolabo ya Nandy na Sho Madjozi kutukona na uwezo wao wa kufanya miziki za kusisimua. Nandy kwa sasa ni mmoja wa wasanii wa kike wanaovuma sana nchini Tanzania.

Nandy anafahamika sana kwa tamasha lake la Nandy Festival ambalo limevutia watu wengi sana. Hapo awali, Nandy alimleta JoeBoy nchini Tanzania kusudi kuwatumbuiza mashabiki katika Nandy Festival.

Leave your comment