S2kizzy: Diamond Ana Zaidi ya Collabo Tatu na Wizkid

[Picha: Targie Griffin Twitter]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtayarishaji muziki kutokea nchini Tanzania Salmin Kasimu Maengo almaarufu kama S2kizzy amethibitisha kuwa bosi wa lebo ya WCB Diamond Platnumz amesharekodi nyimbo zaidi ya tatu na msanii kutokea nchini Nigeria Wizkid.

Mtayarishaji huyo wa wimbo wa ‘Iyo’ kwenye mahojiano yake aliyoyafanya hivi karibuni kwenye Simulizi na Sauti alisema kuwa wasanii hao wakubwa barani Afrika wameshafanya nyimbo zaidi ya tatu na ni suala la muda tu mpaka nyimbo hizo ziachiwe.

Soma Pia: Nyimbo 5 za Kisasa Bongo Zilizochukua Vionjo Kutoka Kwenye Ngoma za Zamani

"Diamond na Wizkid wana nyimbo zaidi ya tatu kwa hiyo zitatoka," alizungumza S2kizzy.

Ni vyema kuweka bayana kuwa kufikia sasa, Diamond Platnumz ameshafanya nyimbo na wasanii wakubwa barani Afrika kama Tiwa Savage, AKA, Davido, Iyanya, Koffi Olomide na wengineo wengi na wimbo huu na Wizkid unategemewa kumuweka Diamond Platnumz kwenye matawi ya juu zaidi.

Aidha, S2Kizzy aliweka wazi kuwa ukaribu wake na msanii Diamond Platnumz umepelekea yeye apate kufahamiana na kufanya muziki na wasanii kutokea mataifa mbalimbali duniani iwe ndani au nje ya Afrika.

Soma Pia: Nyimbo 5 Ambazo Diamond Platnumz Ameshirikisha Wasanii wa Kike

"Naeza nikasema nje wapo (wasanii) Marekani wapo, wapo wengine Netherlands, Marekani, Puerto Rico UK pia nimefanya kazi na wasanii wa UK" alidokeza S2Kizzy.

Kwa siku za hivi karibuni, S2kizzy amekuwa ni mojawapo kati ya watayarishaji muziki ambao wanafanya vizuri sana nchini na hiyo kupelekea yeye kupata umaarufu mkubwa kiasi cha kupata matangazo kutoka kwenye kampuni kubwa ya vinywaji ya Bel Aire kutokea nchini Marekani.

Leave your comment