Nyimbo 5 Ambazo Diamond Platnumz Ameshirikisha Wasanii wa Kike
10 August 2021
[Picha: The Citizen]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Tangu tumfahamu Diamond Platnumz mwaka 2010 kwenye ‘Kamwambie’, Simba bila shaka ametoa nyimbo zaidi ya 100 kwenye kapu lake la burudani na nyimbo zake zote zimependwa na kuvuma sana.
Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii
Ukichunguza kwa umakini kwenye miradi mingi ya Simba, mara nyingi wasanii anaoshirikiana nao ni wa kiume, wa kike ni mara chache sana hivyo basi makala hii inaangazia nyimbo tano ambazo Diamond Platnumz ameshirikisha wasanii wa kike:
Soma Pia: Zuchu Atoa Ushauri kwa Wasanii Chipukizi Wanaotaka Kujikuza Kimuziki
Far Away - Vanessa Mdee
Huu ni wimbo namba 18 kwenye albamu ya ‘A Boy From Tandale’. Diamond Platnumz anampa shavu Vanessa Mdee kwenye wimbo huu ambao ulitayarishwa na S2kizzy. Mashabiki wengi walitegemea video ya wimbo huu kati ya Simba na Cash Madam, lakini inafikia miaka mitatu sasa tangu wimbo huu upikwe lakini hakuna chochote mpaka sasa.
Fire - Tiwa Savage
Tiwa Savage ndiye msanii pekee wa kike kutokea nchini Nigeria kuwahi kushirikishwa kwenye wimbo rasmi na Diamond Platnumz. Bila shaka, Tiwa aliwakilisha vyema nchi yake ya Nigeria kutokana na kuimba vizuri sana kwenye wimbo huu. Wimbo ulitayarishwa na Lizer Classic kutokea Wasafi Records huku video ya wimbo huu ikitayarishwa huko Johanesburg nchini Africa Kusini chini ya Director Nic.
Nitarejea – Hawa
Pamoja na kwamba wimbo huu una umri wa takriban miaka kumi, sauti ya Hawa kwenye aya ya pili ya kibao hiki bado inatukumbusha enzi zile ambapo ukisikia wimbo huu unapigwa redioni au kwenye runinga basi utasimamisha shughuli zako zote ili tu upate maneno matamu ya kibao hiki. "Nitarejea" ulikuwa ni wimbo mkubwa sana na ulimfanya Diamond aende Platnumz lakini kwa Hawa haikuwa hivyo kwani wimbo huu ulipopotea masikioni mwetu na yeye akapotea mazima kutokana na sababu mbalimbali.
Nasema Nawe - Khadija Kopa
Watu wengi hawakuwai kufikiria kuwa ipo siku Simba angeweza kushirikiana na malkia wa mipasho Khadija Kopa kwenye wimbo mmoja kutokana na wasanii hao kufanya haina tofauti ya muziki. Lakini ilipofika Machi 27, 2015, Diamond alionesha kuwa hakuna kitu kinachoshindikana baada ya kutoa ‘Nasema Nawe’. ‘Nasema Nawe’ ilikuwa ni wimbo maarufu sana kiasi cha kushinda kama ‘Nyimbo bora ya Afrika’ kwenye tuzo za Afrimma November 2015.
Baila - Miri Ben Ari
Wimbo namba 9 kwenye albamu yake Diamond ya ‘A Boy from Tandale’. Kwenye wimbo huu, Ben Ari hajaimba lakini ushiriki wake umetokea kwa yeye kucheza fidla kwenye wimbo. Kando na Diamond Platnumz, Miri ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Grammy tayari alishafanya kazi na wasanii wakubwa duniani kama Jay Z, Alicia Keys pamoja na Janeth Jackson. Ilipofika mwaka 2019 wimbo huu ulishinda tuzo ya Africa Entertainment Awards USA kwenye kipengele cha Best Collaboration.
Leave your comment