Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wiki ya pili ya mwezi Agosti imeanza na na kwenye kiwanda cha muziki nchini Tanzania, mambo yanaendelea kuwa sukari sana kwani wasanii wanazidi kuporomosha burudani maridhawa kabisa kukidhi haja za mashabiki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya : Anjella Aachia ‘Nobody Remix’

Kwenye makala hii, tunaangazia nyimbo tano mpya ambazo zimetoka na kutikisa nchini Tanzania:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Anjella Aachia Wimbo Mpya ‘Sina Bahati’

Sio Kitoto – Saraphina

Ndani ya muda mfupi tangu Saraphina atambulishwe rasmi, msanii huyu ameonesha ukomavu wake kimuziki na sasa hivi amekuja upya na ‘Sio kitoto’. Kwenye kibao hiki kilichotayarishwa na Aloney M, Sara kwa kutumia sauti yake tamu anaelezea namna alivyozama kwenye penzi zito na mwandani wake na anaahidi kamwe hawezi kurubuniwa kwa pesa au kitu chochote kumuacha mpenzi wake.

https://www.youtube.com/watch?v=XUrbAdv1RWc

Hatuna Ratiba - Mr Touch ft Billnass, Rapcha & Bau

Kama unataka wimbo wa kukupa hamasa ya kwenda club na kwenye sehemu za starehe basi Mr Touch ametengeneza bidhaa nzuri kwa ajili yako inayokwenda kwa jina la ‘Hatuna Ratiba’. Kulingana na Mr Touch, alianza kwanza kutengeneza kiitikio cha wimbo huu na baada ya hapo akamtafuta Mzee wa Mafioso Billnass aweke verse kisha Rapcha kutokea Bongo Records akapigilia msumari wa ushindi kwenye wimbo huu kwa michano mikali.

https://www.youtube.com/watch?v=h1OJWgfPzQI

Nobody Remix - Anjella ft Country Wizzy, Billnass, Frida Amani na Mabeste

Nobody remix ina maudhui ya mapenzi kama ambavyo toleo halisi la wimbo huu lilivyo, tofauti iliyopo ni kuwa kwa sasa kwenye remix Anjella amepata mrejesho wa kile alichokiimba awali na bila shaka marapa hawa wameweza, kufikisha kile kilichokusudiwa.

https://www.youtube.com/watch?v=cguN31VYLPQ

Cheusi - Kusah

Kwenye ‘Cheusi’, Kusah anamuongelea mwanaume ambaye hana staha na mwenye tabia ya kuongea vitu asivyostahili. Wimbo huu umezua taharuki kubwa sana nchini Tanzania kwani umeonekana kumlenga mojawapo kati ya mastaa wakubwa hapa Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=pRLQFZLe_pQ

Itetemeshe - Bob Junior ft Lavalava

Baada ya kufanya vizuri miaka kadhaa iliyopita Bob Junior amerudi tena kuitetemesha’ tasnia ya muziki hapa nchini Tanzania na kibao chake kipya akimshirikisha bingwa wa nyimbo za mapenzi Lava lava. Baada ya wimbo huu kutoka, Lavalava alikiri kuwa amefurahi sana kupata nafasi ya kufanya wimbo na Bob Junior kwani Junior alikuwa ni mtu aliyekuwa anamuangalia sana kabla hajaanza muziki.

https://www.youtube.com/watch?v=cMJ27cZc8W4

Leave your comment