Nyimbo Mpya : Anjella Aachia ‘Nobody Remix’

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Malkia kutokea lebo ya Konde Gang Anjella ameachia remix ya wimbo wake wa ‘Nobody’ akiwashirikisha wasanii wanne ambao ni; Country Wizzy, Frida Amani, Mabeste pamoja na Young Lunya.

Kwenye remix hii, Anjella kwa sehemu kubwa ameimba kiitikio huku akiwaacha wasanii aliowashirikisha kujinafasi kwenye wimbo huo ambao umetayarishwa na nguli wa muziki B boy Beats.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Anjella Aachia Wimbo Mpya ‘Sina Bahati’

 Country Wizzy anafungua kwenye aya ya kwanza ya wimbo huu kwa michano yake mujarab huku akimwagia sifa kedekede mpenzi aliyeko nae.

"Alafu mtoto ana mshepushepu bhana hilo guu sa hiyo minyamanyama na ka mwili kangu ila ndo tunaendana pole mnaosubiri tutaachana," aliimba Wizzy.

Frida Amani anapokea kwenye aya ya pili ya wimbo na anatumia nafasi yake kutuma ujumbe kwa watesi wake kuwa mwandani wake anampenda sana huku Mabeste na Young Lunya wakinogesha kibao hiki kwa mistari mizito ya rap iliyochanganywa na lugha ya kiingereza.

Soma Pia: Anjella Ashukuru Konde Music Worldwide Kwa Kumkuza Kimuziki

Watu wengi wameonekana kupenda na kufurahia remix ya wimbo huu kwani kwenye ukurasa wa YouTube wa Anjella wachangiaji wengi wametoa mrejesho chanya.

Ni vizuri kuzingatia kuwa wimbo wa ‘Nobody remix’ umeshirikisha wasanii wa Hip-hop pekee. Hii inaturejesha nyuma kidogo mpaka Aprili 18 mwaka huu ambapo Harmonize pia alitoa ‘Bedroom remix’ akishirikisha wasanii wa Hip-hop pekee kama Darassa, Billnass, Country Wizzy, Rosa Ree, na Baghdad.

‘Nobody’ unaendelea kuwa ni wimbo uliomletea mafanikio makubwa sana Anjella tangu kuachiwa kwake na remix hii ambayo kufikia sasa ishatazamwa takribani mara 77,000 kwenye mtandao wa YouTube inatarajiwa kufanya vizuri pia.

https://www.youtube.com/watch?v=cguN31VYLPQ

Leave your comment