Nyimbo Mpya: Anjella Aachia Wimbo Mpya ‘Sina Bahati’

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Anjella kutokea Konde Gang ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Sina Bahati’.

Kwenye wimbo huu, Anjella ameonesha ni jinsi gani mapenzi yanamuumiza kwani mtu anayempenda anaumiza hisia zake hivyo kujiona hana bahati.

Soma Pia: Zuchu Azungumzia Mafanikio Yake Mwaka Mmoja Kwenye WCB

Kwenye aya ya kwanza ya wimbo huu, Anjella anaimba "Wameshakurubuni fadhila zangu huzioni natambua siwezi kung'ang'ana ushanipunguza, bora ungesema kama kuna kosa niliokutendea."

Kufikia sasa wimbo huu uliotengenezwa na mtayarishaji Jerry umesikilizwa na watu elfu sabini na nne kwenye mtandao wa YouTube.

Watu wengi wameonekana kuguswa haswa na wimbo huo kutoka kwa Anjella kwani umewakumbusha maisha yao ya zamani.

Mchangiaji mmoja aliandika "umenifanya nimkumbuke ex wangu wa zamani. Duu ila big song."

Baadhi ya wachangiaji pia walivutiwa na sauti ya Anjella kwenye wimbo huo, kwani kuna mchangiaji mmoja aliandika "the black queen herself teach them good music."

Huu ni wimbo wa nne kutoka kwa Anjella tangu ajiunge rasmi na Konde Gang. Wimbo wake wa kwanza ulikuwa ni ‘Kama’ aliyofanya na bosi wa lebo hiyo Harmonize, kisha akaachia ‘Nobody’, kisha wiki chache zilizopita alishirikiana na msanii kutokea Zanzibar AT kwenye wimbo uitwao ‘Si saizi yao’.

Ikumbukwe pia siku chache zilizopita Anjella alitangaza kutoa remix ya wimbo wake wa ‘Nobody’ ambao anatarajiwa kufanya na wasanii kama Country wizzy, Young Lunya, Billnass, Mabeste na msanii wa Hip-hop Frida Amani.

https://www.youtube.com/watch?v=dfb_TG4eUSo&ab_channel=Anjella

 

Leave your comment