Anjella Ashukuru Konde Music Worldwide Kwa Kumkuza Kimuziki

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Anjella ambaye kwa sasa anatamba katika anga za burudani na ngoma yake ya ‘Sina Bahati’ amechapisha taarifa mtandaoni ambapo amewashukuru wadau mbali mbali walioshirki katika kumjenga kama msanii.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Anjella Aachia Wimbo Mpya ‘Sina Bahati’

Kutokana na sauti yake a kupendeza na ubunifu wa kutunga nyimbo nzuri, Anjella ameibuka na kupata umaarufu mkubwa sana katika tasnia ya muziki ya Afrika Mashariki. Msanii huyo katika chapisho lake mtandaoni aliwatambua baadhi ya watu binafsi wakiwemo Harmonize na meneja wake Uncle Duke.

Anjella pia alitoa shukran za dhati kwa lebo ya Konde Worldwide Music kwa kusimama na yeye kimuziki. Anjella pia hakuwasahau mashabiki wake ambao wamemuunga mkono toka siku ya kwanza na kufanikisha ndoto yake ya muziki.

Soma Pia: Anjella Afichua Wasanii Atakaowashirikisha Kwenye ‘Nobody’ Remix

"Ningependa kumshukuru Mungu kwa kunifikisha hapa, lakini pia naishukuru management yangu @kondegang namshukuru kaka yangu @harmonize_tz na manager wangu @dukeboy_tz kwa support mnayonipa kiukweli sitoacha kuwashukuru lakini pia nawashukuru mashabiki zangu bila ninyi bila support yenu nisingepata hivi ninavyovipata naweza kusema kwa sasa nimeanza kuishi ndani ya ndoto zangu huyu Mungu awabariki," chapisho la Anjella lilisoma.

Anjella hivi karibuni alizawadiwa gari na bosi wake Harmonize. Katika ujumbe wake wa kutoa shukrani, Anjella aliambatanisha picha iliyomwonyesha akiwa ndai ya hilo gari. Mashabiki pia walimpongeza Anjella kwa mafanikio yake katika muziki.

Leave your comment