Anjella Afichua Wasanii Atakaowashirikisha Kwenye ‘Nobody’ Remix

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

 Msanii tajika kutoka Tanzania Anjella ambaye amesainiwa kwenye lebo ya rekodi ya Konde Music Worldwide ametangaza kuwa ataachia remix ya wimbo wake wa Nobody hivi karibuni.

Anjella alipata umaarufu kupitia Konde Music Worldwide ambapo alikuwa amesainiwa na kuungwa mkono na mwanamuziki nyota wa Tanzania Harmonize.

Soma Pia: Harmonize Aanzisha Safari ya Kuinua Mziki wa Zanzibar Kupitia Wimbo Mpya wa Anjella

Baada ya kujiunga na lebo hio, alitoa nyimbo nzuri ambazo zilipokelewa vizuri na mashabiki, kati ya nyimbo zilizofanya vizuri zaidi ni ‘Nobody’.

‘Nobody’ imepokea takriban watazamaji milioni tatu kwenye mtandao wa YouTube tangu uchapishaji wake miezi mitatu iliyopita.

Soma Pia: Sina Chuki na Diamond- AT Aeleza ya Kufanya Kazi na Konde Worldwide

Kufanikiwa kwa wimbo huo kunaonekana kumemsukuma Anjella kutengeza remix yake. Katika taarifa ambayo alichapisha kwenye Instagram Story, Anjella alifunua kuwa atashirikiana na wanamuziki watano kwenye remix ya wimbo huo.

Wanamuziki hao watano watakaoshiriki katika utayarishaji wa remix ya 'Nobody' ni pamoja na; Country Wizzy, Young Lunya, Billnas, Mabeste na Fridah Amani.

Anjella, hata hivyo, hajafichua tarehe halisi ambayo atatoa remix ya ‘Nobody’. Hapo awali Anjella alikuwa amechapisha video ambayo ilimuonyesha akiimba wimbo wa ‘Nobody’ na kufunua kuwa alikuwa akifanya kazi kwa toleo bora la wimbo huo.

"I wish nifanye kitu zaidi ya hiki katika project yangu ijayo," chapisho la Anjella lilisoma.

Leave your comment